Katibu
wa Itikadi ya Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humprey Polepole
(katikati) akisisitiza jambo wakati akitangaza majina ya wagombea wa
nafasi ya Uwakilishi kwa Zanzibar yaliyopitishwa leo na Kamati Kuu ya
Chama hicho, jijini Dodoma. wengine pichani ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya
CCM.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Dodoma
CHAMA
Cha Mapinduzi(CCM) kimetuma salamu kwa vyama vya upinzani kwa kuwataka
kuacha chokochoko na wasioutakia mema nchi yetu huku kikitoa rai kwa
wapinzani kuacha kutaja taja majina ya viongozi wao.
Akizungumza
leo jijini Dodoma ,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM) Humphery Polepole amesema kabla ya kusoma majina ya
wagombea waliopitishwa kugombea ujumbe w baraza la wawakilishi ni vema
kwanza akazungumzia mwenendo wa kampeni unavyoendelea kule Zanzibar na
siasa zake.
Hivyo
amesema kwamba "tungependa kuujulisha umma ya kwamba Chama Cha
Mapinduzi tuko vizuri mno kwa maana ya wana CCM kule , wananchi wa
kawaida kule, ambao wanatuelewa vizuri mno , wameupokea vizuri zaidi
uteuzi wa ndugu yetu Hussein Mwinyi ambaye mpaka sasa hivi tumesema
usikimbie.
",Sasa
hivi anapiga jaramba ya kujiweka sawasawa na sisi tunajua yule ni
kijana ,tena kijana ambaye kwenye uongozi ni bado ana nguvu zake ambazo
wanzazibar wanaweza kuzitumia kwa maslahi mapana ya Zanzibar kwa muda
huu.Lakini tunajua tunao mahasimu wetu ambao hawatatutakii mema na leo
sikutaka kumsema yoyote katika nyumba hii kubwa ya CCM.
"Lakini
nataka kutoa rai mzee yule (ambaye hakumtaja jina) aache kutaja majina
ya viongozi wetu, aache na leo nimetoa heshima kubwa , nimeambatana hapa
na wajumbe wenzangu wa Halmashauri Kuu Taifa Bara na Zanzibar ili haya
ambayo ninawaeleza ifahamike ndio msimamo wa Chama chetu,"amesema
Polepole.
Amesisitiza
ni vema akaachana na anajua Chama Cha Mapinduzi wamepiga hatua na
itakuwa ngumu kwa vyama vingine kupiga siasa ya kueleweka ,wajipange sio
kutengeneza hoja ya kubumba bumba zisizo na mashiko.
",Nimehuzunika
sana mzee yule kwasababu anasema uongo kabisa tena hadharani na sina
hakika huenda anatafuta namna tumshitaki ili apate kiki kwenye uchaguzi
mkuu mwaka huu, hakuna kitu kingine anachotaka zaidi ya kuvuta hisia za
watu.
"Anataka
kutengeneza kitu hivi, kutengeneza umaarufu sisi hatutafanya hivyo
lakini tunamuonya afanye siasa yake,mambo ya CCM atuachie , ziko kauli
ambazo Chama Cha Mapinduzi hatuna tatizo nazo zilishakwisha atuache,ni
vizuri ajifakari afanye kazi ambazo zitakuwa na tija .
"Wapiga
kura wengi ni vijana zaidi na wazee ni wachache ,tunasema kwa mkiki huu
tunaokwenda nao miaka mitano ya kutekeleza ilani tunakwenda mara tatu
zaidi ya ya miaka mitano iliyopita.Basi ni vizuri tukamaanisha watu,
tumekwenda kule Pemba eneo la Mtambwe Taya ambako ndiko anatoka hajawahi
kufanya kitu chochote hata kujenga mnara wa mita moja hajawahi.
"Pale
Mtwambwe Taya kimejengwa kimejengwa chuo cha ufundi stadi na pale
wanafunzi watasoma ,kuna shule ya bweni , ziko bweni za kutosha watoto
karibu 200 watakaa pale watadundishwa ufundi wa aina mbalimbali.Na mambo
hayo yote yamefanyika pale lakini huyu mzee hakufanya chochote, huyu
ameshika nafasi ya uandamizi katika serikali hakufanya chochote.
"Sasa
anatupotezea muda anamsema mgombea wetu , tunasema acha, hii ni mara ya
mwisho,tutashulika na wewe katika namna ambayo inaweza kuleta habari
nyingine, fanya kampeni za kistaarabu na sisi tumezindua kampeni juzi
nzuri kabisa hatutaki kusema watu, tunasema hoja, tunajenga sababu kwa
watanzania,tumepewa heshima kubwa sana katika miama mitano tumefanya
kazi kubwa, kazi imefanyika kule Zanzibar."
Awali
Polepole amesema kama mnavyofahamu leo agosto 31,2020 Kamati Kuu ya
HAlmashauri kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti John Magufuli imeketi jijini
Dodoma ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa mchakato wa uchaguzi mkuu
uliopo mbele yetu.
Amesema
kwamba Kamati Kuu leo imefanya kazi moja kubwa ya kufanya uteuzi wa
mwisho ndani ya Chama."Wanachama wa CCM wanaomba dhamana ya kugombea
kwa nafasi ya ujumbe wa baraza la wawakilishi kule Zanzibar.Kwa nafasi
ya Baraza wa wawakilishi kule Zanzibar.
"Kamati
Kuu chini ya Rais Magufuli imejadili,imetafakari na hamatimaye imefanya
uteuzi wa wana CCM, watu hodari,watu mabingwa kwa maana ya uongozi,
watu ambao ni kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar na mustakali wake wa
sasa na baadae uko katika mikono salama.
"Uamuzi
wa Kamati Kuu siku ya leo umezingatia uwakilishi wa kimakundi kwa maana
makundi rika.Tunaangalia mazingira ya Zanzibar,maisha ya leo kwa
kutizama uchumi wa Zanzibar na hivyo msingi wa kuangalia watu wanaoweza
kuwa na mawazo mazuri yenye kujenga,"amesema.
Ameongeza
kwamba Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa
katika chombo hiki cha dola na wawakilishi Zanzibar linapata wawakilishi
ambao wanasadifu maoni ya Cha Cha Mapinduzi ,maono ya Serikali ya
Jahamhuri ya Muungano wa Tanzania,maono ya mgombea wa chama cha
mapinduzi kul zanzibar ndugu yetu dk.husein mwinyi.
"Tumeshajifafanua
kwamba suala la maendeleo kule Zanzibar sio la mjadala lakini mwendo
kasi wa kuyapaleka maendeleo hayo kwa watu wetu kule Zanzibar halina
mjadala,tumefanya utafiti mkubwa , na tumejiridhisha watanzania
wazanzibar wanataka ule mziki wa ndugu Magufuli katika Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Basi
mziki ule uwakisiwe kule Zanzibar kwa kupitia mtu mmoja,mtaratibu,mpole
mnyenyekevu,mtu wa watu, mwenye nidhamu ya hali ya juu ambaye amehudumu
katika dhamana ya uongozi kama kiongozi mwandamizi ,katika Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ndugu yetu Hussein Mwinyi anaweza
kutuvusha, kuwafikisha mapema zaidi wazanzibar kule tunakotaka kufika
kama Zanzibar na sehemu ya Jamhuri ya Muungano waTanzania,"amesema.
No comments:
Post a Comment