Benki ya NMB katika Maonesho ya Nane Nane - Simiyu - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 3, 2020

Benki ya NMB katika Maonesho ya Nane Nane - Simiyu


Makamu wa Rais - Mh. Samia Suluhu akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB - Benedicto Baragomwa ni jinsi gani benki hiyo inavyoisadia sekta ya kilimo nchini, alipotembelea banda lao katika maonesho ya Nane Nane Mkoani Simiyu. Katika kuendeleza kilimo na kuwainua wakulima, mwaka huu NMB imetenga TZS bilioni 1.9 zitakazotumika kwa ajili ya kujenga maghala ya kuifadhia mazao eneo ambalo Serikali imetenga.


Wakulima wakipata elimu ya kibenki na AgriBiashara katika banda la NMB kwenye maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji - Angela Kairuki (kushoto) na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga (aliyevaa kofia nyekundu) wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi - Sospeter Magesse (kulia), walipotembelea banda la NMB kwenye maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Afisa Utawala NMB kanda ya Magharibi - Julieth Kishamba, akitoa maelezo kwa wateja kuhusu huduma za benki hiyo wakati wa maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. 
Afisa Ushirika wa NMB Foundation - Expedito Nyakunga, akitoa maelezo ya namna ya kumiliki Trekta kwa wananchi waliotembelea banda la NMB kwenye maonesho ya Nane Nan yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad