HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 25, 2020

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI MBIO ZA HISANI ZA CRDB BANK MARATHON

Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB ambao wapo katika Klabu ya wakimbiaji ya Benki hiyo (CRDB Jogging Club) wakiwa katika picha ya pamoja wakati madhimisho ya mwaka mmoja wa klabu ya wakimbiaji ya Kigamboni.

Na Mwandishi wetu.
Kuelekea mbio za hisani za Benki ya CRDB "CRDB Bank Marathon", klabu ya wakimbiaji ya Benki ya CRDB imeendelea kufanya mazoezi na uhamasishaji kwa wakimbiaji na watu mbalimbali kujitokeza kushiriki katika mbio hizo ambazo zina lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia upasuaji kwa watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo alisema ushiriki wa klabu hiyo ni katika maazimisho hayo ni sehemu ya uhamsishaji wa jamii kujitokeza kwa wingi kuchangia matibabu kwa watoto hao wenye magonjwa ya moyo.

"Watoto zaidi ya 500 wanasuburia matibabu ya upasuaji wa moyo katika Taaisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Ni wajibu wetu sisi kama Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwasaidia kupitia CRDB Bank Marathon."

Akielezea namna ya kujisajili na kushiriki katika CRDB Bank Marathon, Kiondo alisema washiriki wanatakiwa kutembelea tovuti maalum ya crdbtz.co/marathon na kisha kufuata hatua chache za kujisajili kwa mtu binafsi na vikundi.

“Kujisajili ni rahisi sana, unaweza kujisajili binafsi na kuchangia shilingi 30,000 au kupitia vikundi na kuchangia 25,000 kwa kila mmoja kupitia matawi ya Benki ya CRDB, CRDB Wakala, SimBanking App na mitandao ya simu (M-Pesa, TigoPesa, AirtelMoney). Fedha hizi zote zitaelekezwa katika kusaidia gharama za upasuaji wa watoto wenye magonjwa ya moyo,” alisema Kiondo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad