HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 21, 2020

TIMU 5 KUFAIDIKA NA VIFAA VYA MICHEZO KILA MWEZI KUTOKA PARIMATCH


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KATIKA kukuza sekta ya michezo, kampuni ya Parimatch imezindua rasmi kampeni ya "Amsha Ndoto na Parimatch" ambayo kila mwezi kutakuwa na droo Maalum itakayowezesha timu shiriki kujipatia vifaa vya michezo kutoka kwao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana amesema lengo la kuanzisha kampeni hii ni kukuza, kuhamasisha na  kutimiza ndoto za vijana katika sekta ya michezo hususani mpira wa miguu.


Amesema, utaratibu utakaotumika ni kwa timu hizo kutembelea tovuti yao na kujaza fomu ya ushiriki na viambatanishw atakavyoelekezwa na kila mwezi timu 5 zitapata vifaa mbalimbali ikiwemo jezi, viatu, mipira na bibs.


"Ili timu hizi ziweze kupata nafasi zitatakiwa kutembelea tovuti yetu ya https://pma.bet/amshandoto kujaza fomu ya ushiriki na viambatanisho husika na kila mwezi tutachagua timu hadi 5 za zitakazopatiwa vifaa ikiwemo jezi, viatu, mipira na bibs."amesema Maligana

 Aidha, ameeleza kuwa kama kila mwezi zitatoka timu tano hivyo kwa mwaka watafikia karibu timu 60 jambo ambalo sio dogo katika kukuza sekta hii ya michezo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana akizungumzia uzinduzi rasmi wa kampeni ya "Amsha Ndoto na Parimatch" ambayo kila mwezi timu tano zitafanikiwa kupata vifaa vya michezo kutoka kwao.











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad