RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NANGULUKULU, SOMANGA MKOANI LINDI WAKATI AKITOKEA MSIBANI MASASI MKOANI MTWARA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 30, 2020

RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NANGULUKULU, SOMANGA MKOANI LINDI WAKATI AKITOKEA MSIBANI MASASI MKOANI MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na zawadi yake ya Jogoo alilopewa na Shaweji Mohamed Kimbwembwe mkazi wa Somanga mkoani Lindi ambaye alifurahishwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais Magufuli wa kuwaletea maendeleo Wananchi wanyonge. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Somanga Rehema Mikidadi Ngenje Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa Shule hiyo ya Msingi ya Somanga. Katika fedha hizo pia Rais aliagiza mwanafunzi huyo apewe Shilingi laki moja kutoka kwenye fedha hizo mara baada ya kuibua kero ya Shule hiyo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi wa Somanga mkoani Lindi mara baada ya kuwahutubia wakati akitokea Masasi mkoani Mtwara. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi kuhusu ubovu wa barabara ya kutokea Lindi- Somanga wakati alipokuwa akitokea Msibani Masasi mkoani Mwara leo tarehe 30 Julai 2020.Wananchi wa Nangulukulu wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao wakati akitokea Masasi leo Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika barabara ya Nangulukulu-hadi Somanga mkoani Lindi ambapo sehemu ya barabara yake imeharibika vibaya na kuhitaji matengenezo makubwa .

PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad