HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 8, 2020

MATUKIO KATIKA PICHA KATIKA BANDA LA TRA SABASABA


 Afisa Takwimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Laban Masunga akimuelezea Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA Dkt. Suleiman Missango (katikati) kuhusu takwimu za makusanyo tangu mwaka 2015 hadi 2020 wakati Mwenyekiti huyo alipotembelea Banda la TRA kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Suleiman Missango akifafanua jambo kwa baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo wakati alipotembelea Banda la TRA kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akifafanua jambo wakati Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo (wa pili kulia) alipotembelea Banda la TRA kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Suleiman Missango akizungumza na baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo wakati alipotembelea Banda la TRA kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).
 Afisa Msimamizi wa Kodi Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Levina Shirima akimhudumia mteja wakati wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).
 Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Godfrey Kumwembe akimhudumia mteja wakati wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).
 Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Martine Malima akiwahudumia wateja wakati wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Bw. Yusuph Aslam akiwaelezea wateja kuhusu umuhimu wa Vilabu vya Kodi katika Shule za Sekondari na Vyuo ya Elimu ya Juu wakati wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba). PICHA ZOTE NA TRA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad