MAGEREZA YARUHUSU WANANCHI KUANZA KUTEMBELEA WAFUNGWA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 30, 2020

MAGEREZA YARUHUSU WANANCHI KUANZA KUTEMBELEA WAFUNGWA

BAADA ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 nchini, Jeshi la Magereza limetoa ruhusa ya kutembelea mahabusu na wafungwa kama ilivyokua awali kuanzia Agosti mwaka huu.

Akizungumza jijini Dodoma leo ,Msemaji wa Jeshi la Magereza SSP Amina Kavirondo amesema walisitisha shughuli za kutembelea wafungwa kutokana na uwepo wa ugonjwa huo lakini kuanzia Agosti 1 ni ruksa kutembelea wafungwa na mahabusu.

SSP Kavirondo amesema wageni wanaoenda kutembelea wafungwa hawapaswi kuzidi wawili na wanatakiwa kwenda kati ya Jumamosi na Jumapili na mazungumzi yasizidi dakika tano na wenye vibali vya kuleta chakula italazimika kuletwa na mtu mmoja.

" Tunashukuru serikali yetu chini ya Rais Dk John Magufuli kwa namna ambavyo imefanikiwa kudhibiti ugonjwa huu na kuruhusu shughuli zote kuendelea kama kawaida, tuwaombe wananchi wanaokuja kutembelea wafungwa wafuate kanuni na taratibu uliowekwa.

Mambo mengine ni pamoja na wageni wote wavae barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni wanapoingia eneo la Gereza na wanapongia gerezani,kuwa umbali wa mita moja kati ya mfungwa/mahabusu na mgeni  lazima uzingatiwe na mazungumzo ya kisheria kati ya wakili na mteja wake yasizidi saa moja," Amesema Kavirondo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad