HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 14, 2020

Dkt Kazi awataka TIC Kujituma

Na Grace Semfuko, Dar Es Salaam
Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC Dkt Maduhu Issac Kazi amesema ubunifu, nidhamu na kujituma ndio njia pekee ambayo itakifanya kituo hicho kuleta ufanisi katika kazi masuala ambayo amepanga kuyasimamia.

Dkt Kazi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Viongozi na Wafanyakazi wa TIC Julai 13, 2020, aliporipoti rasmi kwenye kituo chake kipya cha kazi alichopangiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Julai 12 mwaka huu.

“Kwa uwezo wangu nitakuwa nahamasisha zana ubunifu, kujituma na nidhamu, Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC imekuwepo muda mrefu, kina tamaduni zake na tuziishi tamaduni hizo, yaani kwamba ukiongea na mtu au watu lazima waseme huyu anatoka TIC” alisema Dkt Kazi.

Alisema kutokana na Tanzania kuingia kwenye nchi ya uchumi wa kipato cha kati, wafanyakazi wa kituo hicho hawana budi kuendana na kasi ya hatua hiyo kwa kufanya kazi kwa bidi na nidhamu, ili kufanikisha adhma ya Serikali ya utendaji kazi wenye viwango.
“Nchi yetu imeingia katika uchumi wa kipato cha kati, ni hatua kubwa sana, sote tunafahamu kuwa tumefikia hatua hiyo miaka mitano kabla ya wakati tuliojiwekea, kwa hiyo tuchape kazi na utendaji wetu lazima ubadilike uendane na uchumi huo, ili hata aina ya wawekezaji tulionao wajiweke tofauti na wale tuliowazoea wakati tukiwa kwenye kipato cha chini, tunatakiwa tujiongeze ili tuendane na hatua ya uchumi huo”alisema. 

Alisema ni ushirikiano tu ndio utawezesha kufikia mafanikio ya utendaji kazi wa Kituo hicho na kuzitaka taasisi zinazoshirikiana na TIC kufanikisha uwekezaji, kuboresha na kuimarisha mifumo ya utendaji kazi wao. 

“Kikubwa ni kwamba tuchape kazi, tushirikiane na kama kuna changamoto zozote tuendelee kuwasiliana, hiki chombo ni mtambuka, yaani  ni kwamba humo ndani kuna taasisi mbalimbali ambazo zinashirikiana,mfano TRA, BRELA, OSHA na nyinginezo,naomba tuwe kitu kimoja kwa lengo la kuisaidia TIC na wakati huo huo, mtimize  wajibu wenu kwenye taasisi zenu mlizotoka” alisema Dkt Kazi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad