HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 8, 2020

Aliyekuwa DC Wanging’ombe ,mkoani Njombe atangaza nia ya kugombea ubunge Kilwa Kusini




Na Amiri Kilagalila, Njombe

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe  Ndugu Ally Kasinge ametangaza nia ya kuingia katika mchakato wa kula za maoni wa kumpata mgombea wa ubunge  kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi jimbo la Kilwa Kusini

Kasinge ameweka wazi nia yake mapema siku ya leo wakati akizungumza na vyombo vya habari kwa minajili ya kumshukuru  Mh,Rais  Magufuli kwa kumuamini na kumteua kusimamia halmashauri ya wilaya ya Wanging;ombe  mpaka siku ya jana July 7 alipoteuliwa Lauteri Kanoni  kuwa mkuu wa wilaya hiyo.

“Kabla ya hotuba ya Rais baada ya kuapisha wateule wale ambao aliwaapisha majuzi,ilikuwa ni ngumu kidogo kutafsiri maana halisi ya Mh Rais anakusudia nini kwa sisi wateule wake”alisema Kasinge

“Mimi binafsi tayari nilikuwa ninamatamanio ya kufikiria kufanya utaratibu wa kwenda kwenye Chama changu cha Mapinduzi kwenda katika mchakato kwa kura za maoni,lakini Mh Rais aliweka wazi kwamba  yeye hazuii wateule wake kwenda kuomba kibali au kuomba ruhusa na kuingia katika mchakato wa kisiasa.na alichokuwa anakielekeza kwamba watu wazingatie taratibu waombe ruhusa kwakwe,anatoa ruhusa na baada ya hapo nafasi ambayo alikuwa amekupa anamkabidhi mtu mwingine”alisema Kasinge

Aidha amesema kutokana na maelezo ya Mh Rais ya mala kwa mala juu ya wateule wake haikuwa ngumu kwake kuandika barua ya kuomba kibali kwake.

 “Hatua yangu ya kuandika barua kwa Mh,Rais kuomba kibali ilikuwa ni hatau ambayo nimeifanya kwa moyo mkubwa na hasa nikiamini kuwa kazi ambayo amenikabidhi kuwatumikia wananchi wa Wanging’ombe  kwa kipindi ambacho nimefanya cha miaka minne kwa kifupi nimeifanya kwa ukamilifu wake kama kulikuwa na mapungufu ni ya kibinadamu lakini hakuna binadamu ambaye ni mkamilifu”Alisema Kasinge

Vilele Kasinge amemshukuru Mh,Rais kumuamini na kumuacha katika wilaya hiyo moja ya Wanging’ombe kwa kipindi cha miaka minne.

Katika hatua nyingine Kassinge amesema yuko tayari kuwatumikia wananchi wa Kilwa Kusini kwa njia nyingine kwa kuwa anaamini upinzani ulipata nafasi kuanzia mwaka 2010 kutokana na changamoto zilizokuwemo ndani ya Chama cha Mapinduzi.

“Seleman Bungala maarufu kama Bwege aliingia bungeni mwaka 2010 na ndio mwaka ambao mimi kwa mala ya kwanza niliingia katika mchakato wa kura za maoni za Chama cha Mapinduzi jimbo la Kilwa kusini lakini kutokana na utaratibu ambao haukuwa mzuri kwa wakati huo,ulitoa fursa kwa wapinzani hasa kwa wakati huo chama cha Cuf kuchukuwa jimbo la Kilwa kusini”alisema tena Kasinge

Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli jana Julai 07,2020 alifanya uteuzi wa Mkuu wa wilaya mmoja na wakurugenzi wa Halmashauri watano katika mikoa mbalimbali. 

Rais Magufuli alimteua Lauteri Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe akichukua nafasi ya Ally Kasinge,ambapo kabla ya uteuzi huo Kanoni alikuwa Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Serikali za Mitaa huko Mkoani Songwe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad