HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 2, 2020

NBC YATAMBUA MCHANGO WA POLISI, WAMZAWADIA KOPLO MSOKE FEDHA TASLIMU

Benki ya Biashara ya NBC imempongeza na kutambua juhudi mahususi za Jeshi la Polisi Tanzania na maofisa wake katika kupambana na mlipuko wa homa kali inayosababishwa na virusi vya Covid-19 maarufu kama corona. Katika kipindi chote maofisa kwa Jeshi la Polisi Tanzania wameonyesha hekima ya hali ya juu na dhamira ya kuwatumikia, kuwalinda na kuhakikisha Watanzania wanatekeleza maelekezo ya wataalam ya jinsi ya kupambana na ugonjwa wa corona. 

Aidha, benki hiyo ikishirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania pia imemtambua na kumpongeza Koplo 
Brown Twaibu Msoke kwa kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa katika kupambana 
na gonjwa la corona. 

Koplo Msoke alijizolea umaarufu baada ya video ikimuonyesha akiwahimiza abiria kwenye daladala kufuata maelekezo ya serikali kama kuvaa barakoa, kutosimamisha abiria kwenye usafiri wa umma na kukaa umbali wa mita moja siyo kwa kujilinda tu bali kuwalinda na wengine. 

Akiongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Mawasiliano wa NBC David Raymond amesema“Kufikia maamuzi ya kumpongeza Koplo Msoke ilikuwa kitu rahisi kwa benki yetu, hususani kwa sababu vitendo vyake vya kishujaa vinaendana na msimamo wa benki yetu katika kupambana na virusi vya Covid-19.” 

Amesema Itambulike kuwa Benki ya NBC pia imechukua hatua madhubuti kupamba na kuenea kwa virusi hivyo kama kuwa benki ya kwanza kuweka vitakasa mikono katika ATM zake 

zote nchini, utekelezaji wa nafasi ya mita mbili katika matawi yake na itaendelea kuwahamasisha na kuwaelimisha wafanyakazi wake na Watanzania kwa ujumla jinsi ya kumpambana kwa ugonjwa huyo. 

Aidha RPC Ilala Zuberi Chembera amesema, “Koplo Twaibu ameonyesha mfano mzuri wa kuhamasisha jamii juu ya uvaaji wa barakoa kwa dhumuni la wananchi kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona. Kitendo hicho ni mfano wa kuigwa na kinahitaji pongezi ya pekee hususani kipindi hiki ambacho dunia nzima inapambana na janga hili.

Pamoja Benki ya NBC kumtunuku Koplo Brown Msoke fedha taslim TSHs. 1,000,000 na kumfungulia akaunti katika benki hiyo, Jeshi la Polisi Tanzania pia limemzawadia Koplo Twaibu kiasi cha TSHs 
200,000 na cheti maalumu kutoka kwa Kamanda wa Polizi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa


Katika kuendeleza dhamira ya kuelimisha jamii matumizi sahihi ya barakoa, Benki ya NBC imezindua kampeni yake mpya ya #NBCBarakoaChallenge. Pamoja kuhimiza uvaaji wa barakoa, kampeni ya #NBCBarakoaChallenge itakayoendeshwa kupitia mitandao ya kijamii ya NBC inaangalia pia kuwakumbusha na kuelimisha Watananzania juu ya umuhimu wa kuzingatia tabia kinga ili kuzuia Covid-19.
Koplo Brown Twaibu Msoke akipokea mkono wa pongezi ya fedha taslimu milioni moja kutoka Mkuu wa mawasiliano wa Benki ya NBC David Raymond kwa kuhamasisha jamii juu ya uvaaji wa barakoa kwa dhumuni la wananchi kujikinga na kuwakinga wengine dhidi yamaambukizi ya virusi vya Korona, katika hafla ndogo iliyofanyika katika kituo cha polisi chaSalender Bridge.
RPC wa Ilala Zuberi Chembera akimkabidhi Koplo Brown Twaibu Msoke cheti cha pongezi kwa kazinjema aliyoifanya ya kuelimisha jamii juu ya uvaaji wa barakoa kwa dhumuni la wananchi kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya Korona, katika hafla ndogo iliyofanyika katika kituo cha polisi cha Salender Bridge.







No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad