HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 10, 2020

Dkt. Chaula aipongeza TCRA kwa mafanikio udhibiti wa mawasiliano nchini

 Katibu Mkuu wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Mawasiliano Dkt.Zainabu Chaula akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali katika mamlaka hiyo.
 Katibu Mkuu wa Mawasiliano Dkt.Zainabu Chaula akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Mhandisi James Kilaba kuhusiana na mtambo wa kuangalia masafa wakati alipotembea Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Mkuu wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Mawasiliano Dkt.Zainabu Chaula akipewa maelezo kutoka kwa Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Victor Kweka namna ya mtambo wa kuangalia masafa unavyofanya kazi ,jijini Dar es Salam.



*Watendaji wa TCRA ni wenye ueledi na uzalendo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa imefikisha mawasiliano ya huduma ya simu za mkononi kwa asilimia 94 huku jitihada zikiendelea kufanyika katika kuelekea uchumi wa viwanda.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Mawasiliano Dkt.Zainabu Chaula wakati alipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuangalia utendaji wa mamlaka hiyo na kijifunza mbambo mbalimbali.

Amesema kuwa watangulizi waliopita wamefanya kazi kubwa katika kuisamamia TCRA kwa kupata mafanikio makubwa.

Dkt.Chaula amesema kuwa watendaji wa TCRA ni watu wenye weledi pamoja na uzalendo katika kutekeleza majukumu yao licha ya uchache wao hivyo wanastahili kupongezwa.

Hata hivyo amesema kuwa serikali inaendelea kushughulikia anuani za makazi ambapo uratibu wake umeshaanza kuratibiwa.


Aidha amesema kuwa kutokana na jitihada za TCRA katika udhibiti wa mawasiliano hayo yameweza kuchochea uchumi na kufanya sekta hiyo kuendelea kukua kwa kasi na kwenda sambamba na Teknolojia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad