HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 28, 2020

Kila mmiliki wa Radio lazima kufuata Sheria,Kanuni pamoja miongozo- TCRA Kanda ya Mashariki

 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akisaini (mwenye miwani ) akisaini leseni ya MVIWATA  FM Radio  kulia  ni Mhasibu wa MVIWATA FM Radio Thamas Tembe  na kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Sheria wa TCRA  Vaolet Eseko katika hafla ya kukabidhiana Leseni ya MVIWATA FM Radio.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero  akimkabidhi leseni ya Radio  Mhasibu wa MVIWATA FM Radio  Thomas Tembe anayeshuhudia ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Sheria wa TCRA Kanda ya Mashariki  Vaolet Eseko katika hafla iliyofanyika ofisi ya kanda ya Mashariki TCRA jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MKUU wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawaasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero  amewataka wamiliki wa vituo vya radio kufuata sheria ,Kanuni pamoja na miongozo mbalimbali inayotolewa na Mamlaka hiyo ili kuweza kuhabarisha, kuburudisha na kuelelimisha wananchi kwa usahihi kwa mujibu wa masharti ya leseni wanazopewa.

Mhandisi Odiero ameyasema hayo wakati akikabidhi  Leseni ya Kituo cha Radio cha MVIWATA kilichopo mkoani Morogoro. Amesema kuwa vituo vya radio lazima vizingatie Kanuni za Maudhui ya Utangazaji; bila kufanya hivyo mamlaka inaweza kuwafutia leseni zao.

Amesema kuwa wananchi wanahitakaji mambo matatu katika maudhui  ya utangazaji ya ambayo ni Kuhabarishwa, Kuburudishwa na pamoja na Kuelimishwa hivyo kwenda tofauti na mambo hayo ni ukiukaji  wa matakwa ya leseni.

Mhandisi Odiero amesema Mamlaka  mpaka wanatoa leseni wanakuwa wameshapitia masuala yote muhimu iikiwemo mazingira ya studio pamoja na mitambo ya kurushia matangazo.

"Tunahakikisha wenye leseni za Utangazaji wanafuata miongozo yote ili kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kwa kuzingatia mahitaji ya eneo husika" amesema Mhandisi Odiero.

Kwa upande wa Mhasibu Mwandamizi wa MVIWATA FM Radio   Thomas Tembe baada ya kupokea Leseni kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji MVIWATA radio Stephen Ruvuga amesema kua wanaishukuru TCRA kwa ushirikiano mzuri na ushauri mbalimbali walioupata tangu walipoanza maandalizi ya uanzishwaji wa radio hiyo.

 Amesema  watazingatia miongozo ya TCRA ya uendeshaji wa Radio pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na michezo na Sanaa  ili kuhakikisha vipindi vyote vinajikita katika kuelimisha, kuhabarisha na kuburudisha.

Tembe alisisitiza kwamba MVIWATA FM Radio itahakikisha vipindi vyake vitawanufaisha Wakulima wadogowadogo , Wafugaji, wazalishaji wadogowadogo na Umma wa Watanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad