HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 21, 2020

BARAZA LA WAFANYAKAZI NFRA PAMBANANENI NA RUSHWA KWA VITENDO-HILDA

Na Mathias Canal, NFRA-Morogoro

WATUMISHI wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili katika Utumishi wa Umma.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro.

Kinanga amewataka wafanyakazi hao kuhakikisha kuwa wanapambana na RUSHWA katika sehemu za kazi.

“Kama mnavyofahamu nchi yetu ni kati ya nchi zinazopiga vita suala zima la RUSHWA mahala pa kazi na katika jamii kwa ujumla. Hivyo ninasisitiza na kuelekeza kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa kutoshiriki katika kutoa au kupokea rushwa” Amekaririwa Bi Hilda

Amesisitiza kuwa mtumishi yeyote atakayejihusisha na kubainika kupokea au kutoa rushwa hatua stahiki na kali zitachukuliwa dhini yake.

“Naomba niwakumbushe kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa Mtumishi yoyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na vitendo vinavyokiuka maadili ya Utumishi wa Umma” Amesema

Amesema kuwa serikali inatambua kuwa watumishi bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao kutoa huduma kwa umma ikiwemo ukosefu wa rasilimali fedha na rasilimali watu wa kutosha, hali inayosababisha kutofikiwa kwa malengo.

Aidha amewahakikishia kuwa, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua changamoto hizo, huku akisema kuwa Wataalam hao katika majukumu yao wanapaswa kutumia uwezo weo katika kuibua mikakati itayosaidia kuwezesha Wakala kutekeleza majukumu yake na kujiendesha kibiashara.

Bi Kinanga ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itaendelea na juhudi za kuhakikisha vyombo vya ushirikishwaji wa wafanyakazi katika taasisi na Wakala vinaimarishwa kwa nia ya kuboresha utoaji huduma bora kwa Umma.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa amesema kuwa katika siku mbili za Kikao hicho masuala mbalimbali yatajadiliwa yanayohusu Wakala na miongoni mwa ajenda hizo ni Kupitia Mpango wa Biashara wa mwaka 2020/2021 (Business Plan), taarifa ya utekelezaji ya robo ya tatu ya mwaka 2019/2020 na kupitia Rasimu ya Miundo mipya ya Maendeleo ya Utumishi.

Lupa amemuhakikishia mgeni rasmi kuwa mambo mengine muhimu yatajadiliwa katika kikao hicho ambapo agenda ya kwanza itawapitisha watumishi katika malengo/mipango ya Wakala, ya pili ni utekelezaji wa majukumu ya Wakala uliofanyika kwa mwaka tulionao na tatu ni mpango wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa lengo ya kuandaa majukumu mapya yanayoendana na Muundo mpya wa Taasisi.

Lupa ameiomba serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kuwasiliana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kwa ajili ya kupatikana kwa wataalamu wa kuendesha mradi wa maghala na vihenge vya kisasa punde vitakapokamilika.

Kadhalika Lupa ameiomba serikali kuiruhusu NFRA kutumia fedha za mradi wa ujenzi wa maghala na Vihenge vya kisasa Mkoani Rukwa kukarabati maghala yaliyopo kwa ajili ya kutumika kuhifadhia mahindi kwani msimu wa ununuzi umekaribia.


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya kwenye ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro.
 (Picha Zote Na Mathias Canal, NFRA)
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya kwenye ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA Ndg Milton Lupa (Kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE NFRA Makao Makuu Mathias Mganga.
Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi-Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya kwenye ufunguzi wa Baraza hilo lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi-Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga kwa ajili ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya kwenye ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA Ndg Milton Lupa (Kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE NFRA Makao Makuu Mathias Mganga (Kulia).

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad