HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 7, 2020

ALIYEKUWA AKITAPELI WATU FEDHA KWA KISINGIZIO CHA KUWATAFUTIA KAZI MIKONONI MWA TAKUKURU

 Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Dodoma, Sosthnes Kibwengo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake leo jijini Dodoma.

Charles James, Michuzi TV.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma inamshikilia Bw Simon Jumbe mkazi wa Kisasa jijini Dodoma kwa tuhuma za kujiita Afisa wa Takukuru kinyume na sheria.

Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma, Mkuu wa Takukuru Mkoani hapa, Sosthnes Kibwengo amesema wamemkamata mtuhumiwa huyo baada ya kumuekea mitego mbalimbali na kunasa Aprili 14 Mwaka huu.

Kibwengo amesema Jumbe amekua akiwatapeli fedha watu mbalimbali kwa kisingizio cha kwamba atawasaidia kupata ajira kwenye Taasisi hiyo ilihali akitambua anatenda kinyume na sheria za Takukuru.

Amesema Jumbe aliwahi kumtapeli Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na Baba yake kiasi cha Sh Milioni 2.4 kwa madai ya kwamba atamsaidia kijana huyo kupata kazi kama msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.

Uchunguzi wa Takukuru ulibaini pia Kumbe amekua akijifanya ni Afisa wa Taasisi hiyo kutoka Wilaya ya Chamwini-Dodoma, ambapo aliwahi kumtapeli binti mmoja kiasi cha Sh Laki Mbili ili amsaidie kupata kazi serikali.

" Mtuhumiwa amekua akifanya makosa haya huku akitambua kwamba ni kosa kisheria. Amewahi pia kumtapeli mtoa taarifa wetu kiasi cha Sh Laki Tatu na Nusu kwa kisingizio cha kumtafutia kazi ya Udereva Takukuru.

Niwatake wananchi wa Dodoma kuwa makini na watu wanaotumia Taasisi mbalimbali kuwatapeli kwa kisingizio cha kuwatafutia kazi na kwamba wanapoona tabia hiyo watoe taarifa kwa mamlaka zinazohusika," Amesema Kibwengo.

Amesema wamebaini kuwa mtuhumiwa amekua akichukua fedha hizo kwa kutumiwa kupitia mihamala ya simu na kwamba wanaendelea na uchunguzi zaidi utakapokamilika watamchukulia hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad