HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 24, 2020

WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU NCHINI KUPATA MKOPO WA SHI. BILIONI 27.40

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akiwasilisha taarifa ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020.

Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imesema kiasi cha Sh Bilioni 27.40 kilitolewa na Halmashauri zote nchini kwa ajili ya mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ikiwa ni asilimia 44 ya bajeti ya wanawake, vijana na wenye ulemavu ambayo ni Sh Bilioni 62.40.

Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo imeongoza kutoa mikopo kwa kundi hilo kwa kuchangia asilimia 134 ya bajeti ya wanawake, vijana na wenye ulemavu. 

Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa kusoma taarifa ya mapato kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selamani Jafo amesema ni halmashauri 34 ambazo zimechangia asilimia 75 na zaidi ya bajeti za wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Jafo amesema halmashauri 51 zimechangia kati ya asilimia 50 hadi 74 na halmashauri 67 zimechangia kati ya asilimia 20 hadi 49 ya bajeti ya wanawake, vijana na wenye ulemavu huku halmashauri 33 zikiwa zimechangia chini ya asilimia 20.

Waziri Jafo pia amezungumzia changamoto za ukusanyaji mapato kwa kipindi tajwa ambapo sababu mojawapo ni halmashauri 16 kuomba kubadilisha bajeti ya mapato ya ndani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuweka makisio yasiyoakisi hali halisi ya mapato yanayoweza kukusanywa.

" Baadhi ya halmashauri zimeweka makisio makubwa na madogo bila kuzingatia hali halisi ya uwezo wa vyanzo vya mapato ya ndani na hivyo kushindwa kukusanya mapato kufikia malengo au kuonekana zimekusanya zaidi.

Lakini pia zipo halmashauri ambazo hazisimamii kikamilifu matumizi ya mashine za kukusanyia mapato (POS), Kushindwa kuweka mikakati madhubuti ya kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo vipya vinavyobuniwa na halmashauri," Amesema Jafo.

Amesema kuna changamoto ya halmashauri zingine ambazo hazisimamii kwa makini matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki na hivyo kusababisha kutopatikana kwa taarifa sahihi na kwa wakati.

Ameitaja mikakati ya kutatua changamoto hizo kuwa ni pamoja na upangaji wa bajeti za mapato ya ndani uzingatie uwezo halisi wa mapato ya kila chanzo, halmashauri zitumie takwimu sahihi katika kuandaa makisio ya mapato ya ndani pia halmashauri ziongeze udhibiti wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato ili kuondoa mianya ya upotevu wa mapato.

" Mikoa inapaswa kuendelea kusimamia halmashauri zao kutoa taarifa kupitia mifumo ya kielektroniki kwa kusisitiza kufanyika kwa usuluhisho wa taarifa katika mifumo mbalimbali na kusafisha takwimu chafu kwenye mfumo wa Epicor 10.2 ili kuwezesha kuwa na takwimu sahihi kwenye Dashboard ya mapato ya ndani.

Ofisi ya Rais-Tamisemi imeendelea kuandaa na kusimamia matumizi ya miongozo mbalimbali ya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato na kuendelea kusisitiza matumizi ya fedha hizo yaelekezwe kwenye vipaumbele vilivyomo kwenye mipango ya bajeti," Amesema Waziri Jafo.

[8:55 AM, 4/24/2020] Othman Airtel: Leo Wale watuhumiwa wa Dawa za Kulevya kilo 292 wanapelekwa Mahakamani asubuhi hii kisutu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad