HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 23, 2020

TAKUKURU yawaonya wanasiasa kutoa zawadi zenye harufu ya rushwa

Na Amiri kilagalila, Njombe
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imewaonya wanasiasa walioanza kujitokeza kwa wananchi kugawa zawadi kabla ya muda wa uchaguzi na kutangaza kuto kusita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Domina Mukama wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha miezi mitatu ya januari hadi machi amesema kuwa tayari kuna baadhi ya wanasiasa wameanza kujitokeza kuwahonga wananchi kinyume cha sheria.

“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi,nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba kuwachagua madiwani,Wabunge na Rais kwa mujibu wa katiba ya Nchi.Taasisi imebaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaokiuka sheria,kanunina taratibu za uchaguzi ambao wameanza kufanya kampeni za kuwashawishi wananchi kabla ya muda unaotolewa kwa mujibu wa sheria”alisea Mukama

Baadhi ya wanasiasa na viongozi wa vyama vya siasa mkoani Njombe akiwemo Edwin Mwanzinga na Alatanga Nyagawa wanakiri kuwa rushwa ina madhara makubwa katika chaguzi mbalimbali lakini wametaka takukuru iangazie macho yao katika vyama vyote vya siasa badala ya kujikita na vyama vichache ili hali uchaguzi unahusisha vyama vyote.

“Sisi kwenye chama chetu cha mapinduzi unapotaka kutoa msaada hutakiwi kutoa kwa kificho,unatakiwa uwasilishe kwenye ofisi za chama upate utaratibu ukienda tofauti na hapo inatafsirika ni rushwa vinginevyo usigombee”amesema Mwanzinga

“Kweny chaguzi zipo dalili za rushwa ni vyema vyombo vya kiserikali katika kipindi hiki vikafanya kazi kikamilifu kwenye vyama vyote”alisema Alatanga

Erasto Ngole ni katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe na Rose Mayemba ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa ambao nao wamewaonya wanachama wao wenye nia ya kugombea kwa kuanza kukiuka kanuni kabla ya mchakato kutangazwa.

Mwezi Oktoba mwaka huu Tanzania inatarajia kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu utakaowahusisha madiwani,wabunge na rais hatua ambayo imetajwa kugubikwa na vitendo vya rushwa katika kipindi kama hiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad