HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 28, 2020

BAKWATA MKOA WA SINGIDA YAWAOMBA WAISLAMU,KUOMBA DUA UGONJWA WA KORONA UWEZE KUTOWEKA

 Ni Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi(CCM) Elibariki Emmanueli Kingu (wa kwanza kutoka kushoto) akimkabidhi Katibu wa Bakwata wa Mkoa wa Singida,Alhaji Buruhani Mlau vitabu vitakatifu vya korani tukufu,vikiwemo misahamu 100 pamoja na juzuu 400 kwa ajili ya kugawa kwenye misikiti ya jimbo la Singida Magharibi.
Baadhi ya vitabu vitakatifu(juzuuu) zilizokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi(CCM)Elibariki Emmanueli Kingu kwa ajili ya kusambazwa kwenye misikiti ya jimbo zima la Singida Magharibi ili waumini wa dini ya kiislamu waweze kuomba dua kwa Mwenyezimungu ugonjwa wa korona uweze kutoweka kabisa.
Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Alhaji Buruhani Mlau(wa kwanza kutoka kushoto) akipokea maelezo mafupi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Emmanueli Kingu kabla ya kukabidhiwa msaada wa vitatu vitakatifu vya korani tukufu kwenye ofisui za Bakwata Mkoa wa Singida, zilizopo kwenye msikiti wa kati, mjini Singida.
(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

Na Jumbe Ismailly Singida      
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida limewaomba waumini wa madhehebu ya dini ya kiislamu Mkoani Singida kuvitumia vitabu vya korani tukufu kusoma na kuomba dua ili Mwenyezimungu aweze kuwaondolea waislamu,watanzania pamoja na duniani kwa ujumla janga la COVID -19 linalosababisha ugonjwa wa korona.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Bakwata wa Mkoa wa Singida,Alhaji Buruhani Mlau kwenye hafla ya kupokea vitabu vya koroni tukufu vikiwepo misahafu 100 na juzuuu 400 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi (CCM),Elibariki Emanueli Kingu kwa ajili ya kugawa kwenye misikiti yote ya jimbo hilo.

“Korona hii katika hivi vitabu ni kwa ajili ya kufanya dua ya kujikinga na ugonjwa wa korona,kwani hakuna binadamu mwenye kuweza kuyaondoa maradhi haya ila ni Mwenyezimungu kupitia korani hii tukufu.”alisisitiza Alhaji Mlau.

Aidha katibu huyo wa Bakwata alifafanua pia kwamba juzuuu hizo alizopokea watoto watasoma,watamjua Mwenyezimungu na Mtume Mohammad (SAW).

“Umenikabidhi leo hii (jana) tarehe 02,Ramadhani ambayo ni siku ya pili ya funga yetu leo,hivyo nitawapa waislamu wote wa jimbo lako la Singida Magharibi na watasoma na kuomba dua katika misahafu hii.”aliweka bayana katibu Mlau.

Hivyo Alhaji Mlau alitumia fursa hiyo kumuomba Mwenyezimungu amjaalie Mbunge Kingu na kutoa wito kwa viongozi au wabunge wengine waige mfano wake wa kutoa kwa ajili ya Mwenyezimungu    

Akikabidhi msaada huo wa misahafu 100 na juzuuu 400 kwenye ofisi za Bakwata Mkoa wa Singida zilizopo kwenye msikiti wa kati,Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi,Elibariki Emmanueli Kingu alisisitiza kuwa kwa kuwa kipindi hiki ni cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani,katibu huyo ndiye atakayesimamia ugawaji kwenye misikiti yote ya jimbo hilo ili waislamu waweze kusoma na kuomba dua ili janga la ugonjwa wa korona liweze kutoweka.

“Kwa niaba yangu,familia yangu,familia ya rafiki yangu Kuwingwa wa Manyoni pamoja na rafiki zetu waliopo Saudi Arabia tuliwaomba watupatie msaada wa juzuu pamoja na korani takatifu kwa ajili ya  kuwasaidia waislamu tunapoelekea mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani waweze kuvitumia vitabu hivi kwenye misikiti yangu yote ya jimbo zima la Singida Magharibi.”alifafanua Kingu

Kwa mujibu wa Kingu endapo waumini hao wa dini ya kiislamu watavitumia vitabu hivyo vitakatifu watamuabudu mungu pamoja na kuiombea serikali inayoongozwa na Jemedari Mkuu,Dkt John Pombe Magufuli na kuendelea kutengegeza mshikamano wa Mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad