HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 5, 2020

SEKTA YA AJIRA IMEBAKI KUWA CHANGAMOTO KIDUNIA,NBC WAPEWA TUZO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulubu Hassan amesema ukosefu wa ajira kwa vijana umebaki kuwa changamoto ya kidunia na kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Amesema Kuhusu mwenendo wa soko la ajira kwa mwaka huu inaonesha zaidi ya watu Milioni 187.7 duniani hawana kazi.

Samia amesema katika Jumuiya ya SADC inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 60 ya nguvu kazi ni vijana hivyo hawana budi kuitumia ipasvyo katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini.

Hayo ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa mawaziri na wadau wa utatu wa sekta ya kazi na ajira kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC).

Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni “Kukuza Soko la Ajira na Mahusiano Mema Sehemu za Kazi kwa Maendeleo Endelevu”

Amesema, katika kuelekea siku ya wanawake duniani sekta ya kazi na ajira kuna mambo mengi ya kuangalia ili kuweza kupunguza udhalilishaji wa wanawake makazini pamoja na kuangalia usawa wa kijinsia katika sehemu za kazi.

Amewaomba viongozi kufanya maamuzi, kuyatakekeleza na kusimamia yale yote yanayoazimiwa na kutolewa maamuzi kwa kushirikiana na wadau wa utatu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi amesema kuwa kwa mwaka huu wamejipanga kuchukua vijana zaidi ya 100 na kuwapatia mafunzo ya uzoefu wa kazi yenye lengo la kuwatengeneza kuwa wanataaluma wa baadae pindi watakapoajiriwa kwenye sekta za kibenki nchini.

Sabi amesema hadi hivi sasa NBC imewapokea jumla ya vijana 146 ambao wamewasambaza katika idara na vitengo mbali mbali ndani ya benki hiyo ambako wanafanyakazi zile zile zinazofanywa na watumishi wao walioajiriwa.

Amesema hadi kufikia Desemba mwaka jana, NBC ilikuwa na jumla ya vijana 81 wanaopata mafunzo ya uzoefu wa kazi na Januari mwaka huu , iliongeza vijana 45 chini ya mpango huo huo na kufikisha jumla ya vijana 126 walioko katika benki hiyo hadi hivi sasa.

"kutokana na utendaji mzuri wa kazi uliooneshwa na baadhi ya vijana hao, NBC imewapa mikataba ya kudumu ya ajira vijana wanne ambao wamepangiwa kazi katika maeneo mbali mbali ya benki,"

"Lengo letu ni kuongeza vijana 100 zaidi mwaka huu wa 2020 chini ya mpango wa mafunzo ya uzoefu wa Kazi. Kiukweli mpango wa Serikali wa mafunzo haya, umewawezesha NBC kuwapata vijana wa kitanzania, wenye taaluma tunazohitaji katika benki yetu, na wanafanyakazi katika idara mbali mbali," amesema.

Hata hivyo kwa mwaka 2018 walipokea vijana 44 na kati ya hao, vijana 39 walipatiwa mikataba ya miezi sita ambayo iliwaweze kujifunza, kupata uzoefu na kufanyakazi kwenye idara na vitengo mbali mbali ndani ya benki yao.

"Nia yetu ni kuwafunza vijana wetu kwa kuwapatia uzoefu na stadi mbali mbali, ili pindi nafasi za ajira zitakapotokea basi iwe rahisi kwetu kuwachukuwa na kwapatia ajira za kudumu," amesema Sabi.

Sabi ameeleza, mpango huu wa mafunzo umefanikiwa kutokana na utaratibu mzuri unaoratibiwa na Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA) ya kuchuja vijana kutokana na misingi mitatu muhimu kama vile juhudi, nidhamu na uadilifu.

Hata hivyo amesema kwa mwaka 2020, tayari vijana tisa wamepatiwa mikataba ya mwaka mmoja mmoja wakiwa chini ya uangalizi wa kuwapatia ajira ya kudumu pindi mikataba yao itakapoisha. 

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama, Waziri wa Kazi, Uwezeshaj, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzu Zanzibar Mouldine Gastico na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC) Dr Stragomena Tax na mawaziri mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi akizungumza katika mkutano wa mawaziri na wadau wa utatu wa sekta ya kazi na ajira kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliohudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu. Mkutano huo uliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu akimpatia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya (NBC) Theobaid Sabi tuzo ya ushirikiano katika mpango mafunzo kwa Vijana unaoratibiwa Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA) wakati wa mkutano wa mawaziri na wadau wa utatu wa sekta ya kazi na ajira kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad