HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 10, 2020

RC TABORA AAGIZA KUKAMATWA KWA WANAOTUMIA VYANDARUA KINYUME CHA UTARATIBU


 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwaongoza viongozi mbalimbali kuzindua kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi.


 Mkuu wa wilaya ya Kaliua, Abel Busala akitoa salamu za Wilaya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi.
Katibu Tawala Mkoa Msalika Makungu akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wa Mkoa wa Tabora jana ili azindue kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi .
 Baadhi ya wakazi wa Kaliua wakiwa katika uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi.


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatatinisibwa akitoa hali halisi ya ugonjwa wa malaria mkoani Tabora wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi.


Na Tiganya Vicent
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaagiza viongozi wa vijiji na mitaa kuwamata watu wote watakutwa wakitumia vyandarua kwa matumizi mengine kando ya kujikinga na mbu.

Alisema matumizi ya vyandarua nje ya kujikinga na mbu yanapingana na juhudi za Serikali za kupambana malaria na kusababisha kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Mwanri alitoa kauli hiyo wilayani Kaliua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi.

Alisema kuwa katika baadhi ya watu wanatumia vyandarua kuvulia samaki katika madimbwi na wengine wanatumia kuzungushia vifaranga vya kuku vishismbuliwe na mwewe.

Mwanri aliongeza kuwa kuna watu wengine wanatumia vyandarua hivyo kwa ajili ya kuzungushia bustani za matunda na mboga mboga ili kuzuia wadudu waharibifu.

Alisema matumizi hayo ambayo ni kinyume cha kujikinga na mbu ni marufuku mkoani na atakayekuwa atachukuliwa hatua.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatatinisibwa alisema mwelekeo wa Serikali ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 ugonjwa wa malaria uwe umetokomezwa.

Alisema takwimu zinaonyesha kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa Mkoa wa Tabora bado ni tatizo ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ina asilimia 16.7 , kufuatia Uyui asilimia 16.1 na Sikonge ambayo ina asilimia 13.9.

Dkt. Rutatatinisibwa alisema Urambo ina asilimia 12.8, Manispaa ya Tabora asilimia 8.9, Halamashauri ya wilaya ya Nzega asimilia 8.7, Nzega Mji asilimia 6.8 na Igunga asilimia 5.6.

Alisema nguvu zaidi zinahitajika katika kupmbana na tatizo la malaria mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad