HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 30, 2020

BENKI YA NMB YAKABIDHI SHILINGI MILIONI 100 KWA WAZIRI MKUU KUPAMBANA NA CORONA

Benki ya NMB katika kudhibiti na kupambana dhidi ya virusi vya Corona imekabidhi shilingi milioni 100 kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kama sehemu ya mchango wake kwa serikali katika mapambano hayo. Waziri mkuu amekabidhiwa fedha hizo na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB-Ruth Zaipuna mwishoni mwa wiki katika ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto) akipokea hundi ya Sh. Milioni 100 kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa nne kutoka kushoto) Kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa Serikali wa NMB Alfred Shao na kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Waziri Mkuu- Kassim Majaliwa akizungumza na uongozi wa Benki ya NMB

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad