CCM KUENDELEA KUTAWALA KAMA VYAMA VYA UPINZANI VISIPOFANYA MARIDHIANO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 9 January 2020

CCM KUENDELEA KUTAWALA KAMA VYAMA VYA UPINZANI VISIPOFANYA MARIDHIANO

MWANAHARAKATI na mwanasiasa aliyewahi kugombea Ubunge mwaka 2015 katika Jimbo la Mkuranga kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Kunje Ngombale Mwiru amesema vyama vya upinzani vinatakiwa kufanya maridhiano ya kisiasa, kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Kunje amesema endapo kama wapinzani watashindwa kufanya maridhiano, itakifanya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuweza kutawala kwa karne nyingine.

"Kuna mambo mengi yanafanywa na baadhi ya viongozi wa juu wa vyama kisiasa nchini, ambavyo si ya kujenga vyama bali kuvibomoa.

"Upo udikteta unaoendelea kwenye vyama vya upinzani tangu ulipoingia mfumo wa vyama vingi, wapinzani tunatakiwa tujitafakari kwa haraka kabla ya Uchaguzi Mkuu," amesema.

Amesema yeye ni mwanasiasa msema kweli na daima ataendelea kusema ukweli kwa maslahi mapana ya Watanzania wapenda haki.

Ngombale amesema katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa nchi ni muhimu kwa wao kujipanga pamoja, ili kuweza kuimarisha nguvu kwa ajili ya  kuweza kupambana na CCM ambayo imeota mizizi.

Amesema ili Watanzania waweze kuviunga mkono vyama vya upinzani ni lazima kwanza vikajitafakari upya, kabla ya uchaguzi huo, ambao kuna uwezekano mkubwa kwa CCM kuibuka na ushindi mkubwa endapo haitafanyika kazi ya ziada.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad