HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 6, 2019

UTAFITI WABAINI KUKU WENGI WANAOUZWA MAENEO MTAANI WAKIDAIWA NI WA KIENYEJI KUMBE SI KWELI

UTAFITI uliyofanywa na Shirika linalohusika na usalama  na Ustawi wa wanyama Duniani (World Animal Protection) umebaini kuwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji si wa kienyeji kama inavyosemwa.

Utafiti huo umebaini kuku hao si wa kienyeji bali ni kuku wa kisasa maarufu kama kuku wa kizungu wanaofungwa majumbani kwa kupewa majani pamoja  na dawa mbalimbali za kuwakuza na kuwafanya kuwa wagumu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti huo uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, Msemaji Mkuu wa Shirika hilo, Victor Yamo alisema utafiti huo ambao ulifanywa Juni hadi Julai mwaka huu katika mikoa ya Arusha na Dar es Salaam umebaini jambo hilo hivyo watumiaji wanapaswa kuwa makini.

Yamo amesema kuku wengi wanauzwa katika mikoa hiyo wamekuwa wakupewa dawa za kuwakuza  ambazo zina madhara kwa binadamu pindi wanapotafuna mifupo yao

"Wakati watu wetu wakitembelea kwenye masoko mbalimbali kuulizia bei ya kuku na wakabaini uwepo wa kuku wa kisasa wengi na mwananchi uuziwa kwa kuambia kuwa ni wa kienyeji jambo ambalo ni uongo," alisema.

Amesema utafiti huo ulifanyika kwa lengo la kujua walaji wananunua nyama za aina gani, kutoka wapi pamoja na  kuangalia kama wanafahamu ubora wa chakula na matumizi ya dawa za wanyama.

"Tunaamini kuwa mteja ataelewa nyama anayotaka kununua au kula inaubora au tatizo kiasi gani itakuwa rahisi kujiepusha nayo na kutafuta kitu kingine mbadala cha kula," alisema

Aidha Yamo amesema kwa sasa Shirika lao linafanya jitihada kubwa kuhakikisha linaimarisha ustawi na haki za wanyama na sheria za kuwalinda wanyama hao zinapitishwa na serikali husika katika kila nchi.

Amesema pamoja na kuyafanya hao wanatoa wito kwa watanzania waanze kuelewa kuwa kama watashindwa kuangalia ustawi wa wanyama hasa wanaoliwa kuna hatari kubwa ya kupotea.

"Ni ukweli uliyowazi kuwa ustawi wa wanyama ni muhimu sana na kwa kutambua hilo tumekuwa tukienda mashuleni kufundisha jambo hilo na masuala ya usalama wa chakula na ubora wa dawa," alisema.
 Mtaalamu wa masuala ya kutetea Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection ,Dkt Victor Yamo akifafanua jambo kwa msisitizo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar,alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utafiti uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, kuhusu kubainika kwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji kumbe si wa kienyeji kama inavyosemwa.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza mtaalamu huyo wa Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection, Dkt Victor Yamo alipokuwa akiendelea kufafanua mambo mbalimbali yahusuy haki na ustawi wa Wanyama nchini Tanzania
Mtaalamu wa masuala ya kutetea Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection ,Dkt Victor Yamo akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar,alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utafiti uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, kuhusu kubainika kwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji kumbe si wa kienyeji kama inavyosemwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad