MAHAFALI YA CHUO CHA AFYA MUHIMBILI- MUHAS YAFANA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 8, 2019

MAHAFALI YA CHUO CHA AFYA MUHIMBILI- MUHAS YAFANA

Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, akimtunuku Deus Charles Buma Digrii ya Udaktari wa Falsafa Doctor Of Philosophy (PhD) katika Mahafali ya Kumi na Tatu ya chuo hicho yaliyofanyika Muhimbili jijini Dar es salaam Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili,  Mariam Mwaffisi

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Jumla ya wahitimu  924  wamemaliza masomo yao katika  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mahafali ya 13 ya MUHAS yamefanyikwa kwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Chuo Rais wa Awamu ya Pili Mstaafu Alhaj Alli Hassan Mwinyi na kwuatunukiwa wahitimu waliomaliza masomo yao mwaka 2019.

Katika wahitimu hao, wanne wamefanikwia kuhitimu Digrii ya yzamivu wa Udaktari wa Falsafa  'Doctor of  Phylosophy'  PHD , na wahitimu 284 wakitunukiwa Digrii ya uzamili (masters) katika fani mbalimbali.

Wahitimu 450 walitunukiwa digrii katika fani mbaimbali na  wahitimu 190 wakimaliza masomo yao ngazi ya Diploma.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamivu wa Udaktari wa Falsafa ya Chuo hicho mmoja wa Wahitimu chuoni hapo.
Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Andrea Pembe akitoa Hotuba yake katikaMahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili. (MUHAS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Mariam Joy Mwaffisi akitoa Hotuba yake katika Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili. (MUHAS)
Mwakilishi wa Wahitimu wa Shahada ya Uzamili na Uzamivu wa Chuo hicho, Roselyne Okello akitoa Hotuba kwa niaba ya wenzake katika Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili. (MUHAS)
Baadhi ya Wahitimu wakiwa katika Mahafali hayo ya 13 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
Baadhi ya wahitimu wa chuo hicho wakila kiapo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe akiongozana na Maprofesa na Wahadhiri wa Chuo hicho katika maandamano kuelekea katika Mahafali ya Kumi na Tatu ya Chuo Kikuu kishiriki cha Afya na Sayansi MUHAS yaliyofanyika  jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, akiwa meza kuu pamoja na viongozi na wahadhiri mbalimbali wakati wa mahafali hayo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katika mahafali ya Kumi na Tatu ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi MUHAS Muhimbili jijini Dar es salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad