Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Neli Msuya (kushoto) akiwa moja ya washiriki wa mbio za Kigamboni International Marathon zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA wameshiriki katika mbio za Kigamboni International Marathon na kuwataka wananchi wajiunge na huduma za maji safi.
Dawasa katika mbio hizo wamewaomba wananchi wa Mkoa wa Kihuduma Kigamboni kujiunga na huduma ya maji safi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa Neli Msuya amesema kwa sasa wameanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi ambapo miradi ya Dawasa imepita kwenye mitaa ya Gezaulole, Kizani, Mbwamaji, Vijibweni kata ya uzunguni.
"Tumefungua mkoa wa kihuduma Dawasa Kigamboni ambapo kuna miradi ya maji imeanza kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo mbalimbali na mingine ikiwa bado inaendelea na ujenzi,"amesema Neli.
Amesema, kwa sasa ofisi za Dawasa zinapatikana kwenye bustani ya Gezaulole na utaweza kupata taarifa za namna ya kuunganishiwa huduma ya maji.
"Utakapofika kwenye ofisi zetu zilizopo Bustani ya Gezaulole utajaza fomu ya kuomba huduma ya maunganisho mapya na ndani ya siku saba utapatiwa taarifa ya siku ambayo fundi atakuja kufanya usanifu na utaunganishiwa maji kwa mkopo,"
Mamlaka Dawasa imekuwa inatekeleza ahadi ya rais ha kufikia asilimia 95 ya watumiaji wa maji kwa mwaka 2020 na mpaka kufikia sasa asilimia 85 ya wakazi wa Dar es Salaam wanapata maji safi kutoka Mtambo wa Ruvu Chini, Ruvu Juu na Visima virefu.
Meneja wa DAWASA Mkoa wa kihuduma Tegeta Boniface Philemon (katikati) akiwa na Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Kinondoni Christian Kaoneka (kushoto) wakati wa Kigamboni International Marathon 2019 Km 10 zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakishiriki mbio za Kigamboni International Marathon zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakishiriki mbio za Kigamboni International Marathon zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo baada ya kumaliza mbio za Kigamboni International Marathon 2019 zilizofanyika leo Jijini Dar


No comments:
Post a Comment