HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 18, 2019

BODI YA WAKURUGENZI WA TANESCO WARIDHISHWA NA UTEKEREZAJI MRADI WA KUFUA UMEME JULIS NYERERE

Na Farida Saidy, Pwani

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la umeme Tanzania Tanesco DKt ALEXANDER KYARUZI amesema bodi yake haita mvumilia mtumishi yeyote  wa shirika hilo atakaebainika kuhujumu mradi  wa kufua umeme wa mwalimu Julias Kambarage Nyerere.

Akizungumza mara baada ya kutembelea shughuli mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa katika mradi huo Dkt KYARUZI ambae ameambana na wajumbe wa  bodi  hiyo  amesema  kwa  sasa bodi imeridhishwa na  kasi inayoendelea  katika mradi huo pamoja na  kuwataka wafanyakazi wote kufanyakazi kwa ushirikiano ili  uweze kukamilika  kwa muda uliokusudiwa.
Aidha ziara hiyo  ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO ya kutembelea shughuli mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa katika mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere uliopo katika mikoa ya Morogoro na Pwani imefanywa leo disemba 17.

 Hata hivyo Mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo makazi ya watumishi, ujenzi wa barabara ,na njia ya kuchepushia maji kwaajili ya ujenzi rasmi wa bwawa hilo,mwenyekiti wa bodi  hiyo Dkt ALEXANDER KYARUZI  amesema wameridhishwa na kazi inayoedelea katika ujenzi wa mradi huo.
Kwaupande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umeme Tanzania, Dkt TITO MWINUKA alisema kuwa kasi wanaoendelea nao wakandarasi inaridhisha na wanatarajia kumaliza mradi huo kabla ya juni 14,2022 ambapo mradi unatakiwa kuwa umemalizika. 

NAE mratibu wa mradi huo mhandisi STEVEN MANDA alisema kuwa    hadi sasa mradi huo umefikia asilimia kumi ya utekelezwaji wake,huku ujenzi wa madalaja ukiwa umefikia asilimia 90,na linguine likiwa limemalizika kwa asilimia mia moja.

Hata hivyo Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo ya wakurugenzi  wa tanesco walioambatana na mwenyekiti huyo akiwemo makamu mwenyekiti wa bodi balozi james Nzagi  na Dkt Gemma Modu wamesema kuwa wapo tayari kushirikiana kwa pamoja  ili mradi huo ukamilike kwa haraka kama ilivyukusudiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad