HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 2, 2019

BENKI YA CRDB YATWAA TUZO YA BENKI BORA TANZANIA, 2019

Benki ya CRDB imetajwa kuwa benki bora zaidi kwa mwaka 2019 nchini na Shirika la habari la Finacial Times la nchini Uingereza kupitia jarida la 'The Banker', katika hafla maalum ya utoaji tuzo iliyofanyika katika hoteli ya Sheraton Grand Park Lane, jijini London, Uingereza.

Akizungumza kuhusiana na tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela alisema  tuzo hiyo ni kielelezo cha ukuaji ambao benki hiyo imeupata katika mwaka huu wa 2019 ambao kwa kiasi kikubwa unachangiwa na maboresho ya huduma kwa wateja na uwekezaji katika mifumo ya kidijitali ambao umesaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma na kusogeza huduma karibu zaidi na wateja.

"Tunajivunia sana tuzo hii. Kipekee kabisa niwashukuru sana wateja wetu kwa kutuamini na kutupa nafasi ya kuwahudumia. Tuzo hii inatufanya kutambua kuwa tuko katika njia sahihi ya kuwapatia wateja wetu huduma zilizo bora, "alisema Nsekela.

Akizungumza kwa niaba ya jopo la majaji wa tuzo hizo, ambalo linajumuisha wahariri wa Financial Times na The Banker, John Everigton alisema kwa pamoja wamechagua Benki ya CRDB kwa sababu ya mafanikio makubwa iliyoyapata katika mwaka wa fedha 2019.

Benki ya CRDB imeendelea kufanya vizuri zaidi mwaka huu 2019 ambapo katika matokeo ya fedha ya nusu ya tatu ya mwaka benki hiyo iliripoti faida ya jumla ya shilingi bilioni 92.16 ukilinganisha na shilingi bilioni 52.25 zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

Akizungumza wakati akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema alisema tuzo hizo ni ishara ya weledi na huduma bora inayotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo.

“Ndani ya Benki ya CRDB tunaongozwa na kauli mbiu inayosema ‘Tupo Tayari’ ikimaanisha utayari wetu wakuhakikisha tunawapa wateja wetu uzoefu ulio bora zaidi pindi watumiapo huduma zetu,” aliongezea Boma Raballa.
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa, akiwa na tuzo ya benki bora Tanzania kwa mwaka 2019 iliyotolewa jijini London, Uongereza. Tuzo hiyo iliyolewa na shirika la habari la Financial Times kupitia jarida la The Banker, aliosimama nao ni wahariri wa jarida hilo, John Everigton (kulia) na Michael Beurke (kushoto).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad