Benki ya CRDB imezindua mikopo maalum kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu
ijulikanayo kama “Boom Advance”, uzinduzi huo umefanyika katika tamasha la
michezo la ‘CRDB Bank – TOT Bonanza’ na kuhudhuriwa na wanafunzi wa vyuo
vikuu mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa Benki
ya CRDB, Stephen Adili alisema huduma ya Boom Advance imelenga katika
kuwasiaidia wanafunzi kutatua changamoto ya kifedha pindi wawapo vyuoni.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukiangalia ni kwa namna gani tunaweza kuipatia
suluhisho changamoto hii ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa inachangia kuathiri
masomo ya wanafunzi,” alisema Adili.
Adili alisema mkopo huo wa Boom Advance unatolewa kidijitali kupitia huduma yetu
ya SimBanking App, ambapo ni njia rahisi itakayowawezesha wanafunzi kufurahia
huduma hiyo wakiwa chuoni bila kutembelea benki jambo ambalo lingeweza
kuingiliana na muda wa masomo. “Tumefanya hivi tukifahamu kuwa wanafunzi
wengi wa vyuo wapo katika kizazi cha kidijitali,” aliongezea Adili.
Ili kupata huduma ya Boom Adavance mwananfunzi anatakiwa kuwa mnufaika wa
mkopo kutoka Bodi ya Mikopo HESLB na kusajiliwa katika mfumo wa Benki wa
utoaji mikopo kidijitali “Digital Disbursment System”.
Akiongelea baadhi ya sifa na faida za Boom Advance Adili alisema mkopo huo wa
Boom Advance unamuwezesha mwanafunzi anaweza kukopa kuanzia TZS 40,000
hadi TZS 120,000 bila riba huku muda wa kurejesha mkopo ukiwa hadi siku 45 tokea
kuchukua mkopo, ambapo alisema muda huo umezingatia mpaka mwanafunzi
atakapo pata mkopo mwengine kutoka HELSB.
Adili alisema katika mkopo huo wa Boom Advance malipo yanafanyika moja kwa
moja baada ya mkopo kuingia kwenye akaunti ya mwananfunzi, lakini pia
mwanafunzi anaweza kufanya malipo (yote/sehemu) mwenyewe bila kusubiri hela
ya mkopo kutoka HELSB kuingia.
Alizungumza kwaniaba ya wanafunzi wa vyuo vikuu mwanafunzi wa Chuo cha Kodi,
Catherine Constatine ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma hiyo ya
Boom Advance huku akisema itakwenda kuwa mkombozi kwa wanafunzi wengi
hususan katika kipindi ambacho wanakuwa wakisubiri mkopo kutoka HELLSB au
pindi wanapoishiwa fedha.
Hivi karibuni Benki ya CRDB pia ilifanya maboresho katika Akaunti ya ya wanafunzi
ya scholar ambapo hivi sasa akaunti hiyo haina makato ya aina yoyote, mwanafunzi
pia anaunganishwa na mifumo ya kidijitali itakayomuwezesha kupata huduma za
benki popote pale alipo ikiwamo TemboCard, SimBanking, Internet banking na
CRDB Wakala.
Tamasha hilo pia liliambatana na michezo mbalimbali ambapo timu za mpira wa
miguu na kikapu za Benki ya CRDB na timu za vyuo vikuu ziliumana vikali.
No comments:
Post a Comment