Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitambulishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela (katikati) kwa Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRD Dkt. Joseph Witts wakati alipowasili kufungua Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini lililofanyika Mkoani Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akihutubia wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
David Jere, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi (CRDB) akihutubia wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka
wakandarasi kutumia mabenki kuchukua mikopo ili kuwawezesha
kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuacha kutegemea malipo ya
awali ya mradi husika ambazo zimekuwa zikichelewa na kufanya miradi
kutokamilika kwa wakati.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika kongamano lililo
andaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wakandarasi ,wazabuni na
wafanyabishara wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, lilifanyika katika
ukumbi wa Benki Kuu, mjini Mtwara. Kongamano hilo lililenga kuwapatia
washiriki hao elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha za mikopo
wanazozichukua kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa, wakandarasi ni sekta muhimu
sana katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini hivyo
wanapaswa kuboresha utendaji kazi wao kwa kuchukua mikopo toka
taasisi za fedha na mabenki. Ameongeza kuwa, changamoto kubwa
inayowakabili wakandarasi wengi ni ukosefu wa mitaji kwa ajili ya
kuendesha miradi mbalimbali ambapo changamoto hiyo huchangia
kutomalizika kwa miradi kwa wakati.
“Benki ya CRDB imewaletea fursa mlangoni, itumieni vilivyo,
changamkieni fursa hizo ili muweze kukuza biashara zenu na kupata
faida zaidi, kuongeza ajira kwa vijana wetu na hatimaye kulipa kodi
stahiki za serikali. Ni matarajio yangu kuwa, baada ya kongamano hili
tutaona utofauti mkubwa kutoka kwa wakandarasi na halmashauri,
ambao wamekuwa wakipitia changamoto katika kukamilisha miradi yao,
kutokana na suala la mapato na ukwasi” alisema Waziri Mkuu.
Mheshimiwa Majaliwa pia alipongeza benki ya CRDB kwa kuwa mstari
wa mbele katika kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa
miondombinu mbalimbali ambayo itasadia kuchochea ukuaji wa uchumi.
Alisema “Benki ya CRDB imekuwa ina fadhili miradi mbalimbali ya
kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika jitihda
zake za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Tunatambua na
kuthamini sana ushikiri wa Benki ya CRDB katika utekelezaji wa miradi
ya maendeleo kama vile mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), mradi
wa umeme wa maji katika bonde la Rufiji (Nyerere Hydro Power Project)
na ule wa kusambaza nishati ya umeme vijijini yaani REA.
Kipekee
kabisa niwapongeze tena Benki ya CRDB kwa utayari wenu, ambao
mmekuwa mkiuonesha katika kuisaidia Serikali, hususan katika
utekelezaji wa miradii mikubwa ya kimkakati”. alisema.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela
amesema kuwa,kongamano hili ni fursa pekee ya kuwakutanisha
wakandarasi, wazabuni na wafanyabisahra ili kuwajengea uwezo na
kuwajulisha fursa mbalimbali za kifedha zilizomo ndani ya benki ya
CRDB, na namna ya kuzitumia fursa hizo ili kukuza miradi na biashara
zao.
“Tuna bidhaa nyingi mahususi kwa ajili ya kundi hili la wateja ikiwamo:
Purchase Order Financing, Contract financing, and Invoice Discounting
ambazo hazihitaji dhamana yoyote kutoka kwa Mkandarasi au mzabuni
pindi anapotaka kukopa. Zaidi ya hilo, Benki pia hutoa mikopo kwa ajili
ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi, magari, mashine, Mabasi na huduma
nyingine kama vile dhamana ya malipo ya awali (Advance Payment
Guarantee), dhamana ya Utekelezaji wa Miradi (Performance
Guarantee), Barua za Mikopo (Letters of Credit), Huduma za Bima na
pia tunatoa mikopo ya muda mfupi kama mitaji ya kufanyia kazi”
alisema.
Naye mmoja wa Wakandarasi Henry Shimo ambaye ni Mkurugenzi wa
kampuni ya Chibeshi constructions Ltd , amesema kuwa, swala zima la
uwezeshwaji wa mikopo hiyo litawasaidia kwa kiasi kikubwa sana
wakandarasi hao kumaliza miradi yao kwa wakati kwani changamoto
kubwa ilikuwa ni mitaji kwa ajili ya kuendeleza miradi yao. Amesema
kuwa, kinachotakiwa kikubwa ni uaminifu wa wakandarasi katika kujua
fedha wanayopewa inahitaji kufanyiwa kazi na kurudishwa kwa wakati.
No comments:
Post a Comment