Afisa uhamiaji akihudumia Mwananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Mji mdogo wa Makambako.

Kampuni za simu wakisajili Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako laini za simu kwa alama za vidole.

Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mji Mdogo wa Makambako.
*************************************
Kufuatia
na kujitokeza kwa wingi kwa wakazi wa Makambako na viunga vyake vya
jirani katika zoezi la kupata namba za vitambulisho vya taifa na
kusajili simu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kushirikiana na Mamlaka ya
vitambulisho vya taifa NIDA na watoa huduma wote wa makampuni ya simu
wameongeza muda wa zoezi hilo ambapo sasa zoezi hilo utafanyika kwa wiki
nzima kuanzia Desemba 2 hadi 6 2019.
Akizungumzia
maendeleo ya zoezi hilo linaloratibiwa na TCRA mkuu wa kanda ya Nyanda
za juu Kusini Mhandisi Asajile John amesema lengo la serikali ni
kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaopata huduma za msingi kwa urahisi
hivyo kuongeza huko kwa siku kunalenga kutekeleza malengo hayo.
Amesema
huo ni muendelezo wa kampeni ya “Mnada kwa Mnada, Karibu tukuhudumie”
iliyoanzishwa na kuratibiwa na TCRA na kushirikisha wadau wengine
inayolenga kutoa elimu ya utumiaji bora na salama wa huduma za
mawasiliano na kuhamasisha usajili wa laini kwa kutumia namba za
vitambulisho vya taifa.
No comments:
Post a Comment