Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mkuu wa
Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero (mwenye miwani)
akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha Chrisdome Ambilikile hati
ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) viliyotolewa
na TCRA katika hafla kiliyofanyika shuleni hapo Kibaha mkoani Pwani.
Mwakilishi
ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani ,Katibu Tawala Msaidizi Abdulahman
Mdimu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano (Tehama) vilivyotolewa na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Shule ya Sekondari Kibaha iliyofanyika
shuleni hapo Kibaha mkoani Pwani.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mkuu wa
Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero akizungumza
kuhusiana na vigezo vilivyotumika TCRA kutoa vifaa vya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (Tehama)katika Shule ya Sekondari Kibaha.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari wa Kibaha Chrisdome Ambilikile akizungumza
kuhusiana na msaada wa vifaa vya Tehama katika shule hiyo katika hafla
ilyofanyika shuleni hapo.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Fredrick Ntobi akitoa maelezo kuhusiana na utaratibu wa utoaji wa vifaa
vya Tehama kwa Mamlaka hiyo katika shule ya Sekondari.
Mwanafunzi
wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Kibaha Samuel Makoye akitoa
maelezo kuhusiana na msaada wa vifaa vya Tehama waliopewa katika shule
hiyo.
Picha kati ya TCRA,Wanafunzi ,Walimu pamoja na viongozi wa serikali Mkoa wa Pwani
************************************
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)imesema kuwa itaendelea kusaidia vifaa
mbalimbali vya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa shule
za sekondari zinazofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa
ili kuweza kuwaanda vijana kuendana na mabadiliko ya sayanasi na
teknolojia .
Akizungumza
na mara baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya Tehama Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo
Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa vifaa vya Tehama wanavitoa kwa shule
zinazofanya vizuri katika matokeo kidato cha Nne na Tano ambapo ni
Kibaha sekondari ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri .
Amesema
kuwa vifaa hivyo vitachochea shule hiyo kuendelea kufanya vizuri kwani
vitabu mbalimbali vinapatikana katika mitandao ikiwemo na marejemeo
mengineyo kwani dunia ndio inakwenda huko.
“Hatutarajii
kuona vijana wetu mnatumia vifaa vya Tehama kinyume sheria kwani sheria
mtandaoni imeanisha makosa hivyo wanafunzi mtakuwa watu wa kutumia
Tehama katika maendeleo ya kufanya vizuri kwa kuendeleza rekodi ya shule
ya sekondari Kibaha”amesema Odiero.
Nae
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Matibu Tawala wa Mkoa Abdulahman Mdimu
amesema kuwa wanashukuru kwa msaada waliotoa TCRA na wanafunzi kutunza
vifaa hivyo.
Amesema
kuwa shule ya Sekondari Kibaha kutokana na kupata kigezo cha kupata
vifaa vya Tehama kuongeza juhudi zaidi kwani kuna shule shindani nazo
zinahitaji vifaa hivyo.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Kibaha Chrisdome Ambilikile amesema kuwa kutokana
na kukua kwa Tehama sasa tunatakiwa kuondokana mfumo wa ufundishaji wa
vitabu na daftari ambapo nchi zingine zilishaanza ufundishaji huo.
Amesema
kuwa shule inajenga jengo kubwa pamoja na kuweka vyumba vya Tehama ili
kukidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo na kuongeza kuwa
TCRA kuendelea kuingalia shule hiyo kwa jicho linguine kwa kuwaongeza
vifaa vvya Tehama.
Mwanafunzi
wa Kidoto cha Sita Samuel Makoye amesema kuwa dunia ya sasa imekwenda
na mabadiliko mbalimbali ya ya Tehama ambapo wanafunzi lazima tufuate
tekonolojia hiyo.
kwani kutumia tofauti na matarajio ni hasara kwani na mtakuwa
No comments:
Post a Comment