Na Chalila Kibuda,Morogoro
Mkuu
wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa Wananchi wote watasajili laini za
simu kwa alama za vidole kutokana na jitihada walizoweka kwa
kushirikiana na wadau katika kufanikisha usajili huo.
Akizungumza
na Wananchi wa Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro, Odiero amesema
zoezi la elimu pamoja na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole
linafanyika katika mkoa wote wa Morogoro kwa kupita kila Kata.
Amesema
katika utoaji wa elimu wanashirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA),Watoa Huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi ,Wakala wa
Usajili wa Vifo na Vizazi (RITA) kwa kupata Wananchi huduma kwa pamoja.
Amesema
Wananchi watumie muda wao kutafuta viambatanisho vinavyohitajika kwa
wadau wengine ili waweze kusajili laini zao kwa alama za vidole.Katika
utoaji elimu hiyo wamepita katika vituo vya radio vya Mkoa wa Morogoro
kutoa elimu hiyo watu kujitokeza kusajili laini za simu kwa alama za
vidole.
Aidha
amesema utoaji elimu unakwenda katika mikoa yote iliyopo katika kanda
ya Mashariki ambapo zoezi hilo lilishamalizika katika Mkoa wa Pwani na
kutaka Wananchi wa Mkoa huo ambao hawana vitambulisho vya Taifa kufanya
utaratibu wa kupata katika Ofisi za NIDA ili waweze kusajiliwa.
Kwa
upande mwananchi Amina Salumu wa Manispaa ya Morogoro amesema TCRA
wamefanya vizuri kuhamasisha kwa kuungana na watoa huduma wote katika
usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Aidha
amesema kuwa tatizo lingine ni wao Wananchi kushindwa kufuata taratibu
za kuweza kupata vitambulisho kwa wakati kwa kizingizio cha majukumu
yao.
Salumu
ameshauri kuwa zoezi hilo lifanyike mara kwa mara ili wote waweze
kujisajiliwa wasisubiri laini zifungwe ndipo waanze kuhangaika.
Mkuu
wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mhandisi Lawi Odiero aliyesimama akiangalia kazi data waliosajiliwa na
Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya Namba waweze
kujisajili laini za simu kwa alama za vidole katika utoaji wa elimu
katika Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
Wananchi
wakisajili laini za simu kwa alama za vidole kwa watoa huduma wa
Kampuni za Simu katika utoaji elimu Kata ya Lukobe Manispaa ya
Morogoro.
Afisa
wa TCRA Kanda ya Mashariki Vaoleth Esseko akimkabidhi kitabu Cha
mkataba kwa Wateja Cha TCRA wakati utoaji elimu Kata ya Lukobe Manispaa
ya Morogoro.
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
Mwananchi akisubiri kupewa namba ya kitambulisho cha Taifa kwa kuangalia mfumo aliyessjiliwa na NIDA.
No comments:
Post a Comment