HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 7, 2019

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Mafia katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mafia katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya kuhamasisha usajili wa Laini za Simu kwa alama za Vidole katika uwanja wa Kilindoni Wilayani Mafia mkoani Pwani.
Mkuu wa Kitengo wa Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA Thadeo Ringo akizungumza na mwananchi wa Mafia katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Mafia.
Wananchi wakisajili laini za simu kwa alama za vidole.
Mwananchi akisoma kitabu cha muongozo cha TCRA

**********************************

Wakazi wa wilaya ya Mafia na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 17 lengo kuu ni nchi nzima kufikiwa na Kampeni hiyo.

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema ni fursa kwa wananchi wa Wilaya ya Mafia kufika katika uwanja wa Kilindoni kwa ajili ya kusajili kwa alama za vidole pamoja na kujiandikisha kupata usajili wa vitambulisho vya Taifa kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano.

Mhandisi Odiero amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole pamoja Huduma zingine za mawasiliano..

Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika huduma za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Mhandisi Odiero amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Hata hivyo amesema kuwakuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa.Amesema TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.“TCRA tutahakikisha tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo” amesema.Mhandisi Odiero.

Odiero amesema kuwa Kampeni hiyo imeanza kwa Mkoa wa Pwani hivyo wilaya zote zitakuwa.Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.
Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad