HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 22, 2019

WAZIRI MKUU AWASILI URUSI KUMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA MKUTANO BAINA YA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AFRIKA NA URUSI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa mkate na chumvi  ikiwa ni utamaduni wa kukaribisha wageni wa Warusi wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sochi nchini humo Oktoba 21, 2019 ambako  anamwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, Asha Mkuja wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Demodedovo uliopo Moscow akiwa njiani kwenda Sochi nchini Urusi kumwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya viongozi wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi, Oktoba 21, 2019. Kushoto  ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Marco Mumwi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Marco Mumwi (kushoto) na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, Asha Mkuja wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Demodedovo uliopo Moscow akiwa njiani kwenda Sochi nchini Urusi kumwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya Viongozi wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi, Oktoba 21, 209.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad