TIB CORPORATE BANK YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 10 October 2019

TIB CORPORATE BANK YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Benki ya TIB Corpotare wamekata keki na kusherehekea kwa pamoja na wateja wao katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.Hayo yamefanyika leo katika matawi tofauti ya benki hiyo yaliyopo Jijini Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.


Akizungumza baada ya kumaliza kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja,Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko wa Benki ya TIB Corporate Theresia Soka amesema kwa mwaka huu wameleta huduma ya JIPANGE inayomwezesha mteja kuweka akiba na kujipatia faida.Amesema, mbali na hilo jukumu lao ni kuona wateja wao wanapata huduma bora za kibenki na sio bora katika mlengo mbalimbali.


Theresia amesema, huduma ya JIPANGE inamuhusu mzazi, mtoto, Kijana, Mzee na hata kama kampuni inayotoa huduma kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad