HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 17, 2019

TAASISI YA BRITISH COUNCIL KUANZA KUTOA KOZI KWA WATOTO

TAASISI ya Kimataiafa ya British Council yakabiliana na changamoto ya watu wengi kutokuwa na ujasiri wa kujieleza mbele za watu  imeanzisha kozi ya lugha ya kingereza kwa watoto na kuwajengea uwezo na kujiamini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha ufundishaji wa taasisi ya kimataifa ya British Council, Doris Likwelile jijini Dar Es Slaam leo, amesema kuwa programu kwaajili ya watoto itazinduliwa Jumamosi ya Oktoba 19,2019.

"Kwa mara ya kwanza  kabisa tunaanza kuwa na kozi za kingereza kwa watoto lakini hii kozi itakuwa zaidi kwa mtoto kujifunza kingereza". Amesema Doris

Amesema kuwa ni jambo nzuri kuanzisha kozi hiyo kwa watoto wa kuanzia miaka sita hadi 11 kwani kwa mara ya kwanza itaanza kutolewa hapa nchini ikiwa  taasisi hiyo ilishaenea kwenye nchi zaidi ya 65 duniani kote.

"Mtoto zaidi ya kujifunza Kingereza  mtoto ataongezewa ujuzi ambao unahitajika kwa karne hii ya sasa ya 21 kwa kufanya mawasiliano pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano na kuwa na mawazo mapana,na kuwawezesha kuwa na ujasiri na kuwa wabunifu". Amesema Doris


Nae Meneja wa Huduma ya wateja na mauzo wa Taasisi ya kimataifa ya British Council, Bernard Mosha, amesema kuwa kozi hiyo kwa watoto itakuwa gharama nafuu na mtihani kwaajili ya kiwango utafanyika bila gharama yoyote yaani ni bure kabisa.

"Naomba niwaondoe wasiwasi wazazi kuhusiana na bei zetu kwani wanawezakufikiri kuwa bei zetu zinaweza kuwa za kimataifa hii ni hapana bei zetu zitakuwa za kawaida kwani tumefanya utafiti na kugundua kuwa wazazi kiwango cha uchumi cha wastani kwahiyo gharaama za kozi hii kwa mtoto itakuwa ni nafuu.

Pia amewaomba mzazi au mlezi kumpele mwanaye katika taasisi hiyo ili mtoto aweze kufanya mtihani wa kiwango kwaajili ya kuweza kujua kiwango chake na kuangalia namna ambavyo wanaweza kumfundish kwa ufasaha zaidi.

Kwa Upande wa Usalama wa watoto Mosha amewaondoa wasiswasi wazazi kwani ni sehemu salama kwa watoto.

Hata hivyo Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil,Richard Watkinson amesema kuwa wazazi wawapeleke watoto wakafundishwe lugha ya Kingereza na waingereza wenyewe.
Amesema kuzi hiyo itakuwa na awamu tatu ambapo mtoto atasoma wakati yupo likizo.
 Mkuu wa kitengo cha Ufundishaji cha taasisi ya kimataifa ya British Council , Doris Likwelile akizungumza na waandhi wa habari kuhusu taasisi hiyo kuanzisha kozi ya lugha ya kingereza kwa watoto na kuwajengea uwezo na kujiamini iliyofanyika katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja na Mauzowa British Council, Benard Mosha  na kushoto ni Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil Richard Fielden-Watkinson.
Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil Richard Fielden-Watkinson akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyojipanga kuwahudumia watoto wataojiunga kwenye kozi za taasisi hiyo wakati wa Taasisi hiyo ilipokuwa inatangaza siku ya kuanzisha kozi ya lugha ya kingereza kwa watoto na kuwajengea uwezo na kujiamini iliyofanyika katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja na Mauzowa British Council, Benard Mosha 
 Meneja wa Huduma kwa wateja na Mauzowa British Council, Benard Mosha akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kuwaondoa wananchi hofu kuhusu malipo ya kozi zitolewazo na Shirika hilo wakati wa kutangaza siku ya uzinduzi wa mafunzo ya kiingereza kw watoto kuanzia miaka 6 hadi 11. Wa kwanza kushoto ni  Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil Richard Fielden-Watkinson  na katikati ni  Mkuu wa kitengo cha Ufundishaji cha British Council Tanzania, Doris Likwelile.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad