MRADI WA MAJI KISARAWE KUZINDULIWA OKTOBA 25 MWAKA HUU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 11 October 2019

MRADI WA MAJI KISARAWE KUZINDULIWA OKTOBA 25 MWAKA HUU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Wananchi wa Kisarawe wako mbioni kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa Kisarawe utakaokuwa na uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya 20,000 mwishoni mwa mwezi huu.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Johm Pombe Magufuli anatajiwa kuuzindua mradi huo Oktoba 25 mwaka huu.Mradi huo wenye thamani ya Bilion 10.6 ukijengwa na fedha za ndani za Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) unatarajia kuanza kufanyiwa majaribio Oktoba 20 ikiwa ni kwa ajili ya kusafisha tanki la maji na mabomba.Dawasa wametumia kipindi cha mwaka mmoja kukamilisha kwa mradi huo wakifuata maagizo ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kupeleka maji Kisarawe wakitumia Mtambo wa Ruvu Juu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema wamefurahi kukamilika kwa mradi huu ndani ya wakati na umetumia mfupi sana wa mwaka mmoja wakitumia fedha za ndani.

Luhemeja amesema, wametumia fedha za ndani kukamilisha mradi huu, wenye urefu wa Km 17 na mtandao wa wa usambazaji Km 33 sambamba na kupeleka maji viwanda sawa na Km 13  na tutaanza kuwasha pampu  zilizopo Kibamba ili  kusafisha tanki na Oktoba 25 Rais Dkt Magufuli atakuja kuzindua.

Akielezea umuhimu wa wateja ndani ya DAWASA, Luhemeja amesema kupitia wiki ya huduma ya kwa wateja lengo kuu la mamlaka ni kuona wanakuwa na wateja karibu zaidi na kuwasihi wale ambao hawajaunganishwa na mtandao wao basi wafike kwenye ofisi za Mamlaka hiyo ili kuweza kupata huduma hiyo kwa mkopo."Sisi Dawasa tuna kauli mbiu yetu kupitia wiki hii ya wateja ambayo ni DAWASA TUNAWAHITAJI 

"Kupitia wiki ya huduma kwa wateja, napenda kuwaomba wananchi wa Kisarawe waanze kuchukua fomu wajiandikishe ili mradi utakapoanza waanze kupata maji safi na salama na wataunganishiwa kwa mkopo na watalipia kidogo kidogo kila mwezi kupitia bili zao,"amesema Luhemeja.

"Wananachi msitapeliwa, kuna ofisi zetu hapa Kisarawe, na kisheria Wilaya Kisarawe, Kibaha, Mkuranga zote zipo chini ya Dawasa, tumeshamleta meneja hapa na mkifika mtajaza fomu zitakazowawezesha kuunganishiwa maji na lengo ni kuona kufikia mwisho wa mwezi huu wananchi wa Kisarawe wanatumia na kunywa maji safi na salama kutoka mtambo wetu wa Ruvu Juu,"

Mradi wa Kisarawe ulizunduliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu mwezi Julai 2018 baada ya maagizo ya serikali kuitaka DAWASA ipeleke maji kwenye mji wa Kisarawe na umetumia takribani mwaka mmoja kukamilika, na mradi huo utawanufaisha wananchi wa Kisarawe na maeneo ya viwanda.
  Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea mradi wa Kisarawe unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli Oktona 25 mwaka huu na kuwaahidi wananchi wa Kisarawe kupata maji safi na salama kufikia mwisho wa mwezi huu.
 Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Miradi DAWASA Ramadhani Mtindasi (Pili Kulia) na Msimamizi wa Mradi wa Kisarawe Mhandisi Ismail Kakwezi wakati wa kutembelea mradi wa Kisarawe eneo lilijengwa booster pump itakayopelekea maji kwenye tanki la Kisarawe lenye ujazo wa Lita Milion 6,
   Ulazaji wa mabomba na mafundi wakiendelea na ukamilishaji wa mradi huo kwa kasi.


    Jengo litakalofungwa Booster Pump itakayokuwa na uwezo wa kusafirisha maji kwenda kwenye tanki la Kisarawe.
 Moja ya Booster Pump itakayofungwa na kusafirisha maji kwenda kwenye tanki la Kisarawe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad