MKUTANO WA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO KITAIFA, WAANZA LEO JIJINI ARUSHA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 8 October 2019

MKUTANO WA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO KITAIFA, WAANZA LEO JIJINI ARUSHA

Naibu Mrajis wa vyama vya Ushirika Tanzania Bw. Charles Malunde amewataka viongozi na watendaji wa Vyama vya Akiba na Mikopo kuendelea kuimarisha utendaji wa vyama hivyo vya Ushirika wa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika hususani katika uendeshaji wa vyama    vya Akiba na Mikopo. 

Bw.Malunde ameyasema hayo katika Mkutano wa kumi wamaadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Kitaifa katika siku ya kwanza ya mkutano huo ulioanza Jijini Arusha leo. Mkutano ulioandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania SCCULT (1992) Ltd.

Mwenyekiti wa SCCULT Dkt.Gervas Machimu akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo amewaomba wajumbe hao kutumia mkutano huo kujadili masuala ya vyama vya Akiba na Mikopo, kubadilishana uzoefu, mawazo na kujifunza mambo ya msingi ya uendeshaji wa vyama hivi ili kuongeza tija na ufanisi katika vyama vyao.

Dkt.Machimu ameeleza mkutano huo umelenga kuwakutanisha Viongozi, wajumbe wa Bodi, Wanachama na wadau wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo ili kujadili kwa pamoja fursa, changamoto na kuchangia mawazo katika kuendeleza vyama hivi vyenye mchango na kuleta suluhisho la Mtaji miongoni mwa wananchi. 

Mwenyekiti alifafanua kuwa Kauli Mbiu ya Mkutano kwa mwaka huu isemayo “Huduma kwa Jamii kufikia ulimwengu” imelenga kuelekeza vyama hivi kuendeleza na kuongeza juhudi za kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa lengo la kuboresha uchumi na kuleta maendeleo. Mkutano huo unaoendelea kuanzia leo tarehe 08/10/2019 hadi 10/08/2019.
Wajumbe wa mkutano wa kumi wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo wakijisajili kwaajili ya kuanza mkutano, Leo jijini Arusha.
Wajumbe wakiendelea kujisajili tayari kuanza mkutano, Jijini Arusha

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad