HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 7 October 2019

MKUTANO MKUU SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII SASA OKTOBA 21

Mkutano wa 14 wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka huu uliopangwa kufanyika  Oktoba 8 hadi 11 umesogezwa mbele na utafanyika tena  Oktoba 21 hadi 24 mwezi huu kwa sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.

Akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mabadiliko hayo Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amesema kufuatia mabadiliko hayo Wizara yake inaomba radhi kwa washirikli na waajiri kuhusu usumbufu uliojitokeza kwani sababu za kusogeza mkutano huo ziko nje ya uwezo wa Taasisi.

Bw. Golwike ameutaja Mkutano wa mwaka wa Sekta hiyo wa mwaka 2018 kuwa wenye mafanikio makubwa kwa kuwa uliongeza wigo wa ushiriki  kwa kuhudhuriwa na wataalam wa maendeleo ya Jamii kutoka Serikali za Mitaa na hata Sekta binafsi, NGOs na Taasisi za Elimu ya Juu na mategemeo yake kwa mwaka huu matarajio ni zaidi ya hapo.

Bw. Golwike amekitaja Chama cha Kitaaluma cha Sekta ya Maendeleo ya Jamii maarufu CODEPETA kuwa kimekuwa msaada mkubwa katika kufanikisha maandalizi ya Kongamano la Wanataaluma hao maarufu Nchini kwa kushirikisha Wizara pamoja na  wadau wengine hapa Nchini.

Bw. Golwike pia ameviambia vyombo vya  habari kuwa Wizara tangu mwaka 2001 imekuwa ikifanya Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Nchini  kwa lengo la kubadlishana uzoefu  na utendaji kazi katika kutekeleza majukumu ya Sekta ya Maendelepo ya Jamii.

Jumla ya Mkutano 13 imekwishafanyika na kuhudhuriwa na wataalam wa Kada ya Maendeleo ya Jamii kutoka Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi za Wizara na Wizara za Kisekta zikiwemo Taasisi za Kiraia hapa nchini.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na waandishi wa habari leo jijini  Dodoma kuhusu kusogezwa mbele kwa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Jamii kutoka tarehe 08-10/2019 mpaka tarehe 21-24/10/2019. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad