HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 22, 2019

BENKI YA TADB, PASS WASAINI MAKUBALIANO KUKUZA MAENDELEO YA KILIMO


mkuu wa Atamizi (incubator) wa PASS, Tamimu Amijee kulia akizungumza na waandishi wa haari jijini Dar Es Salaam mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya PASS na Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB), kwaajili ya uanzisha huduma maalumu ya kusaidia shughuli za kilimo cha biashara kwaajili ya Vijana, wanawake na wajasiliamali.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Maendeleo na Kilimo (TADB), Japhet Justine katikati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wakiingia makubaliano ya uwekezaji katika Mradi wa Ubunifu wa kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti  na Mipango, Dkt. Nyankoma Marwa na Kushoto ni  Mkurugenzi mkuu wa Atamizi (incubator) wa PASS, Tamimu Amijee. 
 Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
IKIWA asilimia 35 ya watanzania ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) imedhamiria kuongeza mitaji kwa miradi mbalimbali ya vijana wanaojishughulisha na kilimo.

Benki hiyo ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali linaloshugulikia Kilimo la PASS wamesaini makubaliano ya kushirikiana katika miradi ya Ubunifu ya kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkugenzi Mtendaji wa wa benki ya TADB, Japhet Justine amesema kuwa makubaliano ya leo ni kuwajengea uwezo wanawake na vijana katika kukuza miradi ya ubunifu ya kilimo.

"Ili kuweza kumgusa mkulima mmoja mmoja wa chini na makundi mbalimbali yanayochangia katika pato la taifa hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo ni vizuri kuingia makubaliano na kushirikiana na taasisi zenye malengo sawa na yetu". Amesema Justine.

Justine amesema kuwa ili kuongeza atamizi la vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo na kuwaongezea  huduma ya fedha ili waweze kukuza mipango na miradi yao.

Amesema kuwa Kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kifedha katika kuongeza na kurahisha upatikanaji na kukutanisha wawekezaji wakubwa katika sekta ya kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo kutarahisha miradi ya kibunifu kuleta maendeleo chanya katika nchin kwa ujumla.

Nae Mkurugenzi wa PASS, Tamim Amijee amesema kuwa taasisi ya PASS itashirikiana vyema na TADB kwa kuwekeza zaidi katika kuandaa program na rasilimali watu za kuwajengea uwezo vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo katika kukuza miradi ya kilimobiashara pamoja na kushirikiana bega kwa bega na TADB katika kufanya tathmini na kutoa misaada ya kiufundi zaidi kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo mara baada ya kumaliza program yao na kukuza miradi yao ya kibunifu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad