HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 11, 2019

BENKI YA MAENDELEO TIB YASAIDIA WASIOONA NA WAHANGA WA SARATANI YA MATITI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili (katikati) akizungumza wakati wa sherehe fupi za kukabidhi misaada kwa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke na Taasisi ya Kusaidia Waathirika wa Saratani - TCS HOPE. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TCS HOPE, Bibi Neema Maimu na kulia ni Katibu wa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke, Bw. Protase Mutakyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili (kushoto) akikabidhi fimbo nyeupe kwa Katibu wa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke, Bw. Protase Mutakyanga (kulia). Katikati ni Meneja Uhusiano na Masoko wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili (kulia) akikabidhi mfano wa hundi kwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TCS HOPE, Bibi Neema Maimu.
Katibu wa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke, Bw. Protase Mutakyanga (aliyesimama) akizungumza wakati wa sherehe fupi za kukabidhi misaada kwa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke na Taasisi ya Kusaidia Waathirika wa Saratani - TCS HOPE. Wanaomsikiliza ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili (kushoto) na Mwanachama wa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke, Bi. Angel Sebastian (kulia).
Katibu wa Taasisi ya Kusaidia Waathirika wa Saratani - TCS HOPE, Bw. Luca Mabena (aliyesimama) akizungumza wakati wa sherehe fupi za kukabidhiwa misaada kwa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke na TCS HOPE. Wanaomsikiliza ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili (kulia) na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TCS HOPE, Bibi Neema Maimu (katikati).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa menejimenti na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa sherehe fupi za kukabidhi misaada kwa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke na Taasisi ya Kuwasaidia Waathirika wa Saratani - TCS HOPE.

Na Mwandishi wetu,

Benki ya Maendeleo TIB imeunga mkono jitihada za serikali katika kusaidia masuala ya afya kwa kuwasaidia fimbo nyeupe 86 Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke na kutoa jumla ya shilingi 2,500,000 kama sehemu ya mchango wa ununuzi wa matiti bandia 2500 kwa wahanga wa saratani ya matiti kwa Taasisi ya - TCS HOPE inayowasaidia waathirika wa saratani hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili amesema kwamba TIB kama Taasisi ya Maendeleo inachukulia ustawi wa watu wenye mahitaji maalumu kama mojawapo ya kichocheo muhimu cha maendeleo.

Ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa sekta ya afya katika kuleta maendeleo ya nchi, Benki ya Maendeleo TIB itaendelea kutoa michango hiyo ili kuwasaidia wahitaji wenye mahitaji maalum ya kiafya pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali katika masuala ya afya.

Amesema kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt.  John Pombe Joseph Magufuli, katika kukuza maendeleo ya sekta ya afya, elimu, utengenezaji ajira na ujasiriamali Benki ya Maendeleo TIB imejipanga kuendelea kusaidia jitihada hizo kwa kuwekeza katika miradi ya kimkakati itayosaidia kuongeza kasi ya maendeleo nchini.

“Lengo letu ni kusaidia jitihada za serikali ili kuongeza kasi ya kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo hususani katika kusaidia nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025” alisema.

Akizungumzia msaada walioutoa, Bw. Singili alisema kuwa fimbo zilizotolewa ni nyenzo na visaidizi muhimu kwa wasioona ambavyo zinamsaidia mtu asiyeona aweze kufanya safari zake popote anapotaka kwenda bila kuathiriwa na watumiaji wengine wa barabara.

“Napenda kuiomba jamii na hasa watumiaji wote wa miundo mbinu ya barabara watembea kwa miguu, madereva wa magari, pikipiki (daladala/bodaboda) watumiaji wa vyombo vyote vya moto kuheshimu fimbo nyeupe na kuwasaidia wasioona wawapo barabarani,” Bw. Singili alitoa wito.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke, Bw. Protase Mutakyanga amesema kuwa mchango uliotolewa na Benki hiyo utasaidia wanachama wake kuweza kuendelea kujishughulisha na masuala ya kujitafutia kipato.

“Mchango huu utatuwezesha kushiriki shughuli za kimaendeleo hasa zitakazo saidia kutuingiza kipato,” alisema.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Katibu wa Taasisi ya Kuwasaidia Waathirika wa Saratani - TCS HOPE, Bw. Luca Mabena aliishukuru TIB kwa mchango huo ambao alisema utasaidia kurejesha furaha kwa kina mama waliothirika na saratani ya matiti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad