WIZARA YAWAPIGA MSASA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII TABORA KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 12 September 2019

WIZARA YAWAPIGA MSASA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII TABORA KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI

 Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima akizungumza na maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora wakati akifungua kikao kazi ya kuwajengea uwezo maafisa hao kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Tabora Bw. Panin Kerika akitoa neno la ukaribisho kwa Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima(wa pili kulia) wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii na waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akielezea hali ya ukatili nchini wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii na waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Violeth Mulyalya akielezea kuhusu wajibu wa wazazi au walezi katika malezi wakati wa wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo kuhusu Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Bi. Frida Edward akichangia mada wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bw. Mabula Bugumba akichangia mada wakati wa wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa MAdawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Mkoa wa Tabora wakti wa kikao cha kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Na Mwandishi Wetu Nzega
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imetoa elimu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu madawati ya Jinsia na Watoto mkoa wa Tabora ili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia ili kukabiliana na vitendo vya kikatili katika jamii.

Akifungua kikao kazi cha Maafisa na Waratibu hao leo wilayani Nzega mkoani Tabora Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Tausi Mwilima amesema kuwa malengo ya kuwa na kikao kazi hicho ni kuwajengea uwezo Maafisa na waratubu hao ili waweze kufikisha elimu ya malezi na makuzi katika jamii.

Bi. Tausi ameongeza kuwa lengo la Kitini cha elimu ya malezi ya familia ni muhimu kwani uwapa wazazi na walezi uelewa na jinsi ya kuendeleza malezi na makuzi yenye matokeo chanja kwa watoto ili kujenga jamii yenye kuwajibika na uzalendo.

Amesisitiza kuwa jukumu la kwanza la malezi na makuzi kwa mtoto ni la mzazi au mlezi katika familia hivyo wazazi au walezi wana wajibu mkubwa wa kuzingatia wanawapa watoto wao malezi na makuzi bora.

Aidha Bi. Tausi ameeleza kuwa Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto katika Halmashauri wanajukumu kubwa kufuatilia na kuhakikisha changamoto za malezi na makuzi zinatatuliwa katika jamii na wazazi wanapata elimu sahihi ya kusaidia kuwajengea uelewa juu ya suala la malezi ya familia.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Tabora Bw. Panin Kerika amesema kuwa suala la elimu ya malezi kwa familia ni muhimu na la msingi ambapo linasaidia katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wenye lengo la kutokomeza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Emmanel Burton amesema kuwa Wizara iliamua kuwa na Kitini cha elimu ya malezi kwa familia kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya ukatili katika familia hivyo elimu juu ya malezi na makuzi itasaidia kupunguza vitendo vya ukatili vinavyofanywa katika familia.

Mmoja wa Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Tabora Bi. Faiza Hassan amesema kuwa masuala ya elimu ya malezi kwa familia ni muhimu sana kwa familia kwani familia nyingi zimekuwa zikifanya vitendo vya kikatili bila kujua kama ni vitendo vya ukatili kwa watoto wao.

Naye Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Uyui Bw. Godwin Masaka amesema kuwa elimu ya malezi kwa familia itawasaidia Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kuwajengea uwezo wa kwenda katika jamii kuwapatia elimu hiyo ili kuimarisha misingi ya malezi na makuzi katika familia.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad