HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 21, 2019

WADAU WA MAJI WATEMBELEA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI WA RUVU CHINI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA wamefanya ziara ya pamoja na wadau wa maji wanaojishughulisha na masuala mbalimbali yakiwemo kilimo cha mboga mboga, bustani, wauzaji wa maua na sehemu za kuoshea magari (car wash) kutoka Mkoa wa Dawasa Tegeta kwenye mtambo wa uzalishaji Ruvu Chini kwa lengo la kuwaonesha maji yanavyozalishwa.



Ziara hiyo imefanyika leo, sambamba na kuwapatia elimu wadau hao wa maji ambao wengi wao ni wateja wa Mamlaka hiyo na kuwataka waende kuwa mabalozi wazuri watakaporejea.

Akizungumzia ziara hiyo, Meneja Mawasaliano DAWASA Everlasting Lyaro amesema wadau hao wa maji ni watu muhimu sana kwahiyi ni muhiku kufahamu maji yanaandaliwaje mpaka kufikia kwa watumiaji majk.

Amesema, anaamini pindi watakaporejea majumbani watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao na kutoa elimu ya namna ya matumizi ya maji ili kutohujumu mamlaka kwa kuharibu miundo mbinu au kuchepusha maji.

"hatutaki kuwa maadui na wateja wetu zaidi tunapenda kuwa marafiki, na lengo la kuwaita pamoja ni kuzungumzia vitu mbalimbali ikiwamo sheria hii mpya ya maji na kutembelea mtambo wetu wa Ruvu chinj na mtaona jinsi maji yanavyozalishwa" amesema Everlasting.

Naye Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Ole Philemon amesema kumekuwa na changamoto kubwa sana kwa wananchi kuhujumu miundo mbinu ila ziara hii iliyoandaliwa kwa ajili ya wadau wa maji itaenda kuzalisha jambo zuri sana na kuwapa nafasi ya kufahamu uzalishaji wa maji mpaka kufikia hatua ya mwisho.

Ole amesema, sheria mpya ya maji iliyosainiwa Julai Mosi 2019 imeelezea makosa ya jinai na adhabu kwa mtu atakayekamatwa anahujumu miundo mbinu ya maji ikiwemo faini siyo chini ya Milion 5 hadi 50 na kifungo kisichopungua miaka miwili hadi mitano.

Kwa upande wa Wadau wa Maji, Mzee Tupa amesema wamefurahi kutembelea mtambo wa Ruvu Chini ambapo uzalishaji mkubwa wa maji na namna Mamlaka inavyotumia gharama kubwa kuanza kuyaandaa mpaka kuyasafirisha kutoka mtamboni hadi wa watumiaji ambapo no Dar es Salaam na baadhi ya Maeneo ya mkoa wa Pwani.

Watumiaji hao wa maji wanajishughulisha na masuala mbalimbali yakiwemo kilimo cha mboga mboga, bustani, wauzaji wa maua na sehemu za kuoshea magari (car wash) ambapo walipewa elimu kutoka Kaimu Mzalishaji wa Maji Abasi Abdallah ambaye aliwaonesha kuanzisha mwanzo hadi mwisho.

Mtambo wa Ruvu Chini ulizunduliwa na Rais Wa Awamu ya kwanza Hayati Mwalimu Julius Nyerere Desemba 8 1976 ukiwa ni moja ya mtambo Mkubwa unaozalisja lita za ujazo Milion 230 kwa siku.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Everlasting Lyaro akizungumza na wadau wa maji wa Mkoa wa Kihuduma Tegeta kuhusiana na elimu ya matumizi ya maji na sheria mpya iliyosainiwa Julai Mosi 2019 inayowataka wananchi kulinda miundo mbinu ya jamii.
Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Ole Philemon akizungumza na wadau wa wa maji wa Tegeta kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Chini na kufahamu namna maji yanavyozalishwa ili wakawe mabalozi wazuri kwa wenzao.
Kaimu Mzalishaji wa Mtambo Ruvu Chini Abasi Abdallah akitoa maelezo kwa wadau wa maji waliotembelea mtambo huo na kuwaonesha kuanzia chanzo cha Maji yanapotokea kwenye Mto Ruvu hadi hatua ya mwisho ya kwenda kwa mtumiaji.
Mmoja wa wadau wa maji akiyanywa maji ambayo yapo tayari kuanza kusafirishwa kwenda kwa mtuamiaji wa mwisho.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad