HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 17, 2019

UBAGUZI NA KUNYANYAPALIWA BADO NI CHANGAMOTO KWA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI NCHINI

   Na Khadija seif, Michuzi tv
TUME ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS) imesema haitosita kushirikiana na makampuni mengi nchini kutoa elimu ya virusi vya ukimwi (VVU)katika shughuli zote za kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi idara ya habari na Mawasiliano Jumanne Issango wakati wakupokea hundi ya milioni 2 kutoka kwa makamo wa rais wa Kampuni ya startimes Bi.zuhura  amesema tume inajisikia faraja na fahari kuona makampuni mengi yanaunga mkono juhudi mbalimbali za kudhibiti maambukizi ya ukimwi.

"Majukumu ya tume ni kutengeneza sera na Mikakati ya kudhibiti ukimwi,kufuatilia na kutathimini ugonjwa huo,kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa afua za ukimwi pamoja na kusaidia juhudi za kutafuta tiba,"

Hata hivyo Issango amefafanua kuwa utafiti wa viashiria vya virusi vya ukimwi (VVU) wa mwaka 2016 hadi 2017 umebainisha kuwa maambukizi mapya ni makubwa kwa kundi la vijana wa umri wa miaka 15 hadi 24.

"Tafiti hiyo inaonyesha kuwa wastani wa idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) kila mwaka ni 72,000,"

Na pia amesema bado  tume hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo sekta ya elimu ya elimu pamoja na afya wameelekeza nguvu zaidi katika kundi la vijana kwa kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa walio mashuleni,vyuoni na hata walio nje ya mfumo wa elimu.

Vilevile amebainisha changamoto wanazokumbana nazo ni pamoja na unyanyapaajwi na ubaguzi kwa watu wanaoishi virusi vya ukimwi (VVU) pamoja  na jitihada za Serikali za kuhakikisha maambukizi yanapungua ifikapo mwaka 2020.

"Pamoja na changamoto ya unyanyapaajwi pia ipo changamoto nyingine ambayo ni upungufu wa rasilimali fedha pamoja na utegemezi mkubwa wa wahisani ,kwani asilimia 93 ya fedha za utekelezaji wa afua za ukimwi unategemea wafadhili wa nje ya nchi "

Pia ameipongeza serikali kwa kuanzisha mfuko wa udhamini wa kudhibiti ukimwi (ATF) kwa lengo la kukusanya rasilimali fedha za ndani kwa ajili ya kuimarisha mwitikio wa udhibiti wa ukimwi nchini.
Mkurugenzi idara ya habari na Mawasiliano Jumanne Issango akipokea hundi ya milioni 2 kutoka kwa Makamo wa rais wa Kampuni ya startimes katika kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi(VVU) nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad