TUWAWEKEZEE WATOTO ELIMU BADALA YA KUWAPA UFAHARI ILI KUINUA TAALUMA ZAO-NDIKILO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 23 September 2019

TUWAWEKEZEE WATOTO ELIMU BADALA YA KUWAPA UFAHARI ILI KUINUA TAALUMA ZAO-NDIKILO

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

WAZAZI, walezi mkoani Pwani, wametakiwa kumpa hazina ya elimu mtoto na kumwekezea elimu ikiwa ni urithi mkubwa wa maisha yake ,badala ya kumpatia vitu vya kifahari kama magari suala ambalo linachangia kurudisha nyuma maendeleo yake kitaaluma .

Aidha watoto wameaswa kuacha kujiingiza katika tabia hatarishi kama vile kutumia madawa ya kulevya ikiwemo bangi na badala yake wawe na hofu ya mungu kwa kufuata maadili mema.

Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alitoa rai hiyo wakati wa mahafali ya 14 ,ya  darasa la saba ya shule ya msingi Kibaha Independent (KIPS )iliyopo Kibaha.

Aliwataka wazazi na walezi wenyewe kumtengeneza mtoto kwa kumuandaa  na kesho yake kwa kumfuatilia muenendo wa masomo yake .

"Muda wa kuwapa magari na simu kubwa za kiganjani utafika , ,Tuwawezeee elimu kwa manufaa yao baadae":-Wanangu safari yenu bado mbichi, elimu ni bahari ,pambaneni ,Tanzania inasubiri vijana wasomi ,msiwe na haraka na mambo ya dunia na ya ovyo ovyo kwani maisha hayataki haraka"alisisitiza Ndikilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wakurugenzi wa NJUWENI na bodi ya shule hiyo, alhaj Yusuph Mfinanga alisema, ili kuepukana na utapeli kwa malipo mbalimbali shuleni hapo wazazi wanapaswa kulipa ada na michango kupitia akaunti ya shule badala ya kukabidhi fedha mkononi .
Awali mkurugenzi wa shule hiyo ,Nuru Mfinanga alieleza, kwa sasa wanafanya upanuzi wa kwa kujenga shule eneo la Mwanalugali ili wanafunzi wanaojiunga shuleni hapo wasikose nafasi kutokana na ufinyu wa eneo la sasa na kuongoza mikondo.

Nuru alibainisha ,wanafunzi wanafanya vizuri kitaaluma kwani mwaka 2016 shule hiyo ilikuwa ya 16 kati ya shule 323, mwaka 2017 ilikuwa ya nne na mwaka 2018 ilikuwa ya nne hivyo mwaka huu wanatarajia kufanya vizuri zaidi .
Jumla ya wahitimu 82 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya msingi kwa mwaka 2019 shule ya msingi KIPS.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad