HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 24, 2019

Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Geita wazinduliwa

Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Geita umezinduliwa jana tarehe 22 Septemba 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa Maonyesho ya Teknolojia ya Dhahabu kwenye Uwanja wa Kalangalala Mjini Geita. Zaidi ya watu 1000 walishiriki uzinduzi huo, ikijumuisha viongozi mbalimbali wakiwamo Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Madau wa Madini.

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu alibainisha jitihada mbalimbali ambazo Serikali imefanya kuhakikisha Madini yananufaisha Nchi na Watu wake.

Waziri Mkuu Majaliwa amewaonya watoroshaji Madini na kusema Serikali ipo makini na imejidhatiti vya kutosha na kwamba haitokuwa na huruma nao. Aidha alisema kwa wale wasiotaka kuelewa na kuacha kutorosha madini Serikali itashughulika nao.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kwa sasa Serikali na Makampuni yanayomiliki migodi wanaheshimiana kwani Makampuni hayo yanatii magizo na kufuata sheria za nchi.

Waziri Doto amesema kabla ya kufunguliwa kwa masoko ya madini nchini makusanyo ya dhahabu yalikuwa kilo 101 kwa mwezi lakini baada ya masoko kufunguliwa makusanyo yameongezeka na kufikia kilo 1,974 hivi sasa.

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, alisema ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kwa kushirikiana na Serikali imekuwa ikiandaa Miongozo ya Uwekezaji katika Mikoa kwa lengo la kuchambua na kuainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika mikoa husika ili kuwavutia wawekezaji.

Dkt. Kida alisema mpaka sasa ESRF imesaidia Mikoa 17 kuandaa Miongozo ya Uwekezaji ambapo mikoa 11 imekamilisha na Mikoa 6 iko katika hatua mbalimbali na kuongeza kuwa ESRF itaendelea kuandaa Miongozo ya Uwekezaji katika mikoa iliyobaki kuanzia mwezi wa kumi mwaka.

Alisema kazi hii ya Uandaaji wa Miongozo ya Uwekezaji imeweza kuibua fursa nyingi kwenye Mikoa husika zikiwa katika sekta na ngazi zote.

"Kwa mfano mheshimiwa Waziri hapa Geita kuna fursa kubwa katika sekta ya madini hasa uchimbaji na uongezaji thamani wa madini ya dhahabu kwa wawekezaji wadogo, wa kati na wakubwa. Fursa nyingine zipo katika sekta ya viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi, ujenzi, utalii, na huduma. Maelezo ya kina juu ya fursa hizo yapo kwenye Mwongozo wa Uwekezaji ambao utauzindua leo hii”alisema Dkt. Kida.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ESRF Miongozo hii ya Uwekezaji ngazi ya Mikoa itachangia katika Mwongozo wa Uwekezaji wa Taifa na kwamba ESRF itaendelea kushirikiana na mikoa katika utekelezaji wa miongozo hii kwa kusaidia kufanya upembuzi yakinifu (feasibilty studies), kuandaa Miongozo ya Biashara (Business Plans) kwa baadhi ya fursa ambazo mikoa itapenda kuwekeza, na kunadi fursa zilizopo kwenye Miongozo.

Aidha Kida alishukuru wataalamu wa ESRF walioshiriki kuandaa mwongozo huo na kuufanikisha. Aliwataja kwa majina waliofanikisha kuwa ni pamoja na Margareth Nzuki, Dk Oswald Mashindano, Prof. Godwin Mjema; Doris Lyimo na Mussa Mayala Martine.

Mkurugenzi wa ESRF aliwapongeza pia viongozi wa Mkoa wa Geita kwa jitihada zao za kuuweka wazi mkoa huo na kuwataka wadau wote kuhakikisha Mwongozo huo unatumika ipasavyo ili kuleta matokeo yaliyo kusudiwa katika mkoa wa Geita na Taifa kwa ujumla.
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri mara baada ya kuwasili kwenye uwanja Kahangalala mjini Geita kwa ajili ya kushiriki kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Geita Mjini, Joseph Kasheku (kulia) maarufu kama Musukuma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja Kahangalala mjini Geita kwa ajili ya kushiriki kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Katikati ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida na Prof. Godwin Mjema ambaye ni mmoja wa watu waliofanikisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita wakielekea kwenye eneo maalum lililotengwa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja Kahangalala mjini Geita kwa ajili ya kushiriki kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel akitoa salamu na kuwakaribisha wageni wakati sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofanyika katika uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
  
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita iliyoandaliwa na taasisi yake kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Maendeleo (UNDP) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu uliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo huo kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Madini, Mh. Doto Biteko (wa pili kushoto) Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi (kulia).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel (wa pili kulia) Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Msanii wa muziki wa Injili nchini Emmanuel Mbasha akitoa burudani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Pili ya Tekinolojia ya Dhahabu na Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Geita uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na wadau wa ESRF na UNDP mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa GGM mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji mkoa wa Geita katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM wa mkoa wa Geita mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa huo hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida na Mkuu wa Idara ya maarifa na Ubunifu wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na mdau wa Geita wakati sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofanyika katika uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofanyika katika uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Kutoka kushoto ni Meneja wa Data wa ESRF, John Kajiba, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri pamoja na wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad