MTOTO WA NAIBU WAZIRI WA ARDHI DAVID NA SANDRA WALIVYOMEREMETA KATIKA SHEREHE YA NDOA UKUMBI WA MALAIKA BEACH RESORT MWANZA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 17 September 2019

MTOTO WA NAIBU WAZIRI WA ARDHI DAVID NA SANDRA WALIVYOMEREMETA KATIKA SHEREHE YA NDOA UKUMBI WA MALAIKA BEACH RESORT MWANZA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula akiwa na mtoto wake David Mabula (wa tatu kushoto) na mkewe Sandra Ndiwu wakisikiliza maelekezo kwa makini wakati wa hafla ya kuwapongeza kufunga ndoa. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

David Mabula na mke wake Sandra Ndiwu wakiwasili katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza kwa ajili ya sherehe ya kupongezwa baada ya kufunga ndoa takatifu katika Kanisa Katoliki la St Joseph Kirumba Mwanza mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifurahia jambo na Sandra Ndiwu (Mke wa mtoto wake) wakati wa hafla ya kusheherekea kufunga ndoa takatifu kwa mtoto wake David iliyofanyika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta akimvisha Khanga Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula kwa niaba ya Wabunge wenzake wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt. Mabula aliyefunga ndoa na Sandra Ndiwu mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika akisalimiana na Masajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Stela Tullo wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula aliyefunga ndoa mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Tutubi Mangazeni.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika (Kushoto) akiongoza watumishi wa Wizara yake kwenda kutoa zawadi wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula aliyefunga ndoa mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara yake wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula aliyefunga ndoa mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
David Mabula mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa hafla ya kumpongeza kwa kufunga ndoa na Sandra Ndiwu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni watoto wa mhe Dkt Angeline Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Urambo mkoani Tabora Magreth Sitta akizungumza kwa niaba ya Wabunge wenzake wakati wa wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kufunga ndoa mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Bendi ya Twanga Pepeta ikitumbuiza wakati wa hafla ya kumpongeza Mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kufunga ndoa mwishoni mwa wiki.

(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad