HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 4, 2019

MAHAKAMA YA KISUTU KUTOA MAAMUZI KESI YA AVEVA NA WENZAKE SEPTEMBA 17 MWAKA HUU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Septemba 17 mwaka huu inatarajiwa kutoa uamuzi wa kama aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva na wenzake wanakesi ya kujibu ama la.

Washitakiwa hao wote wanakabiliwa na mashitaka 10 ikiwemo kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji wa fedha.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya usajiri wa klabu hiyo, Zackaria Hanspoppe na aliyekuwa Makamu wa rais wa klabu hiyo Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu


Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa Septemba 17 mwaka huu mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba anayesikiliza kesi hiyo.

Upande wa mashitaka ukiwakilishwa na wakili wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) , Leonard Swai ,leo umefunga ushahidi wao ambapo jumla ya mashahidi 10 na vielelezo mbalimbali viliweza kutolewa.

Moja ya mashahidi waliotoa ushahidi wao ni mtaalamu wa Maabara ya Sayansi Jinai, Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam ,Faustine Mashauri ambapo katika ushahidi wake amedai Septemba 4 mwaka 2017 akiwa kwenye ofisi za maabara hiyo, alipokea bahasha kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Takukuru iliyokuwa na vielelezo pamoja na bahasha iliyokuwa na maombi ya uchunguzi wa vielelezo hivyo.

Amedai, vielelezo hivyo ni vile vinavyobishaniwa na visivyobishaniwa ambapo vinavyobishaniwa ni hundi lutoka benki ya CRDB na fomu ya maombi ya kuhamisha fedha kutoka benki hiyo kwenda benki nyingine.

Mashauri amedai, vielelezo visivyobishaniwa vilikuwa ni sahihi za majina ya watu wawili ambayo ni jina la Nyange na Aveva, na baada ya kufanya uchunguzi aliweza kubaini sahihi zilizokuwa katika hundi zinafanana na zile sahihi zisizobishaniwa za Nyange na Aveva wanazotumia katika shuguli zao za kila siku.

Amedai kuwa, baada ya kupata uhakika ina maana kuwa Kitaalamu nyaraka zilisainiwa na watu hao na alivyokamilisha uchunguzi,aliandaa ripoti na kuipeleka ofisi za Takukuru.

Katika mashitaka la kughushi linawakabili washitakiwa wote, anadaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.

Pia katika mashitaka mengine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad