HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 16, 2019

MADUMU YA MAFUTA 859 YAKAMATWA BAGAMOYO

Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Wankyo Nyigesa akiwaonesha waandishi wa habari mafuta yaliyokamatwa Bagamoyo.

Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
JESHI la Polisi mkoani Pwani, limekamata madumu 859 ya mafuta ya kula yanayodaiwa kutolipiwa ushuru, yenye thamani takriban milioni 50, huko Chemchem kata ya Magomeni Bagamoyo.

Akithibitisha kuhusu tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani hapo,Wankyo Nyigesa amesema ,madumu hayo yalikuwa yakisafirishwa na Christopher Emmanuel (32).

Alieleza kuwa, Christopher aliyasafirisha madumu hayo kupitia gari yake namba T.621 BCG aina ya fuso baada ya kukwepa kulipa ushuru kwenye moja ya bandari bubu Bagamoyo.

"Tunachunguza risiti zake za malipo kwani pia zina TIN namba tofauti, tunamshikilia mtu huyu pamoja na aliyeshirikiana nae kutoa Hassan Saidi mpemba huyu mkazi wa Bagamoyo."

Wankyo amesema, huo ni usafirishaji haramu na kutia hasara Taifa kwa kukwepa kulipa ushuru ama kodi,hivyo amewaasa wananchi kuacha biashara za magendo.

Kamanda huyo amefafanua, wafanyabiashara wanapaswa kulipa ushuru kwa maendeleo ya Taifa na sio kutaka faida kwa njia za mkato.

Amebainisha hawatawaachia nafasi wakwepa ushuru na kudhibiti mianya ya kukwepa ushuru kwenye bandari zote bubu kwakuwa zinafahamika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad