HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 8, 2019

KAILIMA ARIDHISHWA NA UJENZI JENGO LA IDARA YA UHAMIAJI DODOMA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo wakimsikiliza Mhandisi Issa Mohamed Issa wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019.

Na Mwandishi Wetu-MOHA, Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa 8 la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu, linalojengwa Mjini Dodoma.

Ujenzi huo utagharimu sh. bilioni 30 na unatarajiwa kukamilika Novemba, 2020 ila unaweza kumalizika kabla ya muda huo kama hakutatokea changamoto yoyote. Kailima aliyasema hayo jana alipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya ujenzi huo.

Jengo hilo linajengwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT). Alisema ziara hiyo imelenga kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. John Magufuli juu ya kuhamia Dodoma.

Alifafanua kuwa, SUMA JKT ina Wakandarasi wazuri wenye uzoefu mkubwa kwenye ujenzi wa majengo mbalimbali. “SUMA JKT unapowapa mradi, ujenzi wake huwa unakamilika kwa wakati ndio maana hupewa kazi nyingi za ujenzi wa majengo ya Serikali,” alisema.

Kailima alisema hadi sasa ujenzi umekamilika kwenye hatua ya awali (chini), lengo la Serikali ni kuifanya Idara ya Uhamiaji iondokane na uhaba wa majengo kwenye mikoa mbalimbali.

“Hivi sasa tunaendelea na ukarabati kwenye majengo ya Uhamiaji Mtwara, Lindi, ukarabati mwingine utafanyika Manyara,” alisisitiza Kailima.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (aliyekaa) akisisitiza jambo wakati akipewa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya Uhamiaji, Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019 kutoka kwa Mhandisi Issa Mohamed Issa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (watatu kushoto) na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo, wakimsikiliza Mhandisi Issa Mohamed Issa alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima akisisitiza jambo wakati akipewa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad