DIAMOND PLATINUMZ APEWA UBALOZI WA PARI MATCH TANZANIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 12 September 2019

DIAMOND PLATINUMZ APEWA UBALOZI WA PARI MATCH TANZANIA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ ameteuliwa na kutambulishwa leo kama balozi wa Kampuni ya michezo ya kubashiri Pari March Tanzania.

Mkurugenzi muendeshaji wa Parimatch Tanzania 
Tumaini Maligana amesema wamechukua hatua ya uthubutu na kumchagua Diamond kama balozi wetu kwa dhana hii (Burudani),yeye ni mtu ambaye amepambana na ameweza, Ila kikubwa ni kwamba huwezi ongelea burudani Tanzania bila kumtaja Diamond.

Kama balozi atasaidia kutoa uelewa kwa wachezaji maana hasa ya kubeti ili wote tuweze kufurahi na kucheza kistarabu.

Maligana amesema kwa msaada toka kwa Bodi Ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ambao wamekua mstari wa mbele katika kuhakikisha wanasimamia na kuhimiza kubeti kistarabu kupitia kampeni yao ya Makinika kijana, wanaahidi kuwaunga mkono katika hili kwa manufaa ya watu wote na kwa wateja wetu.

Amesema kuwa, kuna  Ofa na Promosheni zinakuja, Kama bado hujawa Mwanafamilia wa Parimatch Huu ni wakati wa kuungana nasi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msanii Diamond amesema anachofahamu ni kwamba kwa upande wa Pari Match Kubeti sio ajira ni burudani,na ndio maana wameweka mkazo katika kubeti kistarabu.

Akitolea mfano wa burudani, Diamond amesema ukienda kwenye show ya mziki unakua na kinywaji na utatokelezea basi hata ukitazama mpira, weka mkeka wako kuongeza msisimko na shangwe .

Amesema, yeye na menejimenti yake wamedhamiria kuwapeleka washindi wale wanaopata donge nono kwenda kushuhudia mechi nje ya nchi na sio kuishia kubeti tu.

“Mimi na Menejimenti yangu tunasafiri sana, na tulikua tunajadili namna ya kuwasapoti washindi hao na kuonelea kuwapeleka kushuhudia mechi hizo nje ya nchi hasa wale waliopata donge nono na sio kuishia kubeti tu,”amesema Diamond.

Bodi ya Michezo Nchini imeweka mikakati ya kuwasajili wachezaji wote wanaocheza michezo ya kubashiri, ambapo itasaidia katika kutambua umri sahihi wa mshiriki na kucheza kwa ustaarabu.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wake kama Balozi wa Kampuni ya Kubashiri ya Pari Match uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Pari Match Na Menejimenti ya Wasafi wakati wa hafla ua kumtambulisha kama Balozi wa Kampuni ya Kubashiri Pari Match Tanzania leo Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad